Friday, February 12, 2021

MKURABITA INA MCHANGO MKUBWA UJENZI WA UCHUMI ZANZIBAR-RAIS DKT.MWINYI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisisitiza umuhimu wa Mpango wa Kurasimisha Rasiliamli na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) katika kuleta ukombozi wa kiuchumi na kuondoa migogoro ya ardhi visiwani Zanzibar wakati Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango huo (Hawapo pichani) walipomtembelea   Ikulu Jijini Zanzibar leo Februari 11, 2021 na kueleza hatua iliyofikiwa katika urasimishaji ardhi na biashara  visiwani humo.

Wajumbe wa  Kamati ya Uongozi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wakifuatilia hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi  walipomtembelea Ikulu Jijini Zanzibar na kufanya naye mazungumzo kuhusu hatua iliyofikiwa katika urasimishaji ardhi na biashara visiwani humo.

Makamu  Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge  Tanzania (MKURABITA) Bi. Immaculata Senje akieleza mikakati ya mpango huo ikiwemo kupima viwanja 5700, kujenga vituo jumuishi  vya Biashara vipatavyo  10 katika wilaya mbalimbali za Unguja na Pemba wakati wajumbe wa Kamati hiyo walipomtembelea Ikulu Jijini Zanzibar leo Februari 11, 2021 na kueleza utekelezaji wa Mpango huo tangua kuanza kwa shughuli za urasimishaji visiwani humo.

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge  Tanzania (MKURABITA) Dkt. Seraphia Mgembe akieleza kuhusu namna wananchi wa Zanibar wanavyounga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar katika kuwaletea ukombozi wa kiuchumi ikiwemo kuwezesha urasimishaji ardhi na biashara unaofanywa kupitia MKURABITA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge  Tanzania (MKURABITA), Watumishi na Menejimenti ya Mpango huo  leo Ikulu Jijini Zanzibar mara baada ya kukutana na Kamati hiyo.

(Picha  zote  na MAELEZO)

……………………………………………………………………..

 
Na‌ ‌Mwandishi‌ ‌Wetu-‌ ‌Unguja‌ 
Rais‌ ‌wa‌ ‌Zanzibar‌ ‌na‌ ‌Mwenyekiti‌ ‌wa‌ ‌Baraza‌ ‌la‌ ‌Mapinduzi‌ ‌Mhe.‌ ‌Dkt.‌ ‌Hussein‌ ‌Ali‌ ‌Mwinyi‌ ‌amesema‌ kuwa‌ ‌Mpango‌ ‌wa‌ ‌Kurasimisha‌ ‌Rasilimali‌ ‌na‌ ‌Biashara‌ ‌za‌ ‌Wanyonge‌ ‌Tanzania‌ ‌(MKURABITA)‌ ‌una‌ ‌ mchango‌ ‌mkubwa‌ ‌katika‌ ‌kujenga‌ ‌uchumi‌ ‌na‌ ‌kuondoa‌ ‌migogoro‌ ‌ya‌ ‌ardhi‌ ‌baada‌ ‌ya‌ ‌urasimishaji.‌  
Ameyasema‌ ‌hayo‌ ‌leo‌ ‌Februari‌ ‌11,‌ ‌2021‌ ‌Ikulu‌ ‌Jijini‌ ‌Zanzibar‌ ‌wakati‌ ‌alipokutana‌ ‌na‌ ‌kufanya‌ mazungumzo‌ ‌na‌ ‌wajumbe‌ ‌wa‌ ‌Kamati‌ ‌ya‌ ‌Uongozi‌ ‌ya‌ ‌MKURABITA‌ ‌na‌ ‌Menejimenti‌ ‌ya‌ ‌Mpango‌ ‌ huo.‌ 
“Nimejulishwa‌ ‌kuwa‌ ‌Mpango‌ ‌huu‌ ‌tangu‌ ‌uanze‌ ‌hapa‌ ‌Zanzibar,‌ ‌tayari‌ ‌shilingi‌ ‌milioni‌ ‌441‌ 
zimetolewa‌ ‌kuwezesha‌ ‌urasimishaji,‌ ‌naahidi‌ ‌kwamba‌ ‌Serikali‌ ‌ya‌ ‌Mapinduzi‌ ‌Zanzibar‌ ‌itaendelea‌ 
kutoa‌ ‌kipaumbele‌ ‌kwa‌ ‌kutenga‌ ‌bajeti‌ ‌ili‌ ‌kuendekeza‌ ‌kazi‌ ‌hii‌ ‌ya‌ ‌urasimishaji‌ ‌”,alisisitiza‌ ‌Rais‌ Dkt.‌ ‌Mwinyi‌  
Akifafanua‌ ‌amesema‌ ‌kuwa‌ ‌mpango‌ ‌wa‌ ‌urasimishaji‌ ‌utasaidia‌ ‌wananchi‌ ‌wengi‌ ‌zaidi‌ ‌kupata‌ mitaji‌ ‌ya‌ ‌kukuza‌ ‌biashara‌ ‌na‌ ‌shughuli‌ ‌za‌ ‌uzalishaji.‌  
Aidha,‌ ‌Mhe.‌ ‌Rais‌ ‌Mwinyi‌ ‌amesema‌ ‌Serikali‌ ‌ya‌ ‌Mapinduzi‌ ‌Zanzibar‌ ‌itafanyia‌ ‌kazi‌ ‌mapendekezo‌ yaliyotolewa‌ ‌na‌ ‌Makamu‌ ‌Mwenyekiti‌ ‌wa‌ ‌Mpango‌ ‌huo‌ ‌Bi.‌ ‌Immaculata‌ ‌Senje‌ ‌ikiwemo‌ ‌kuendelea‌ ‌kutenga‌ ‌bajeti‌ ‌ya‌ ‌urasimishaji.‌  
“Mapendekezo‌ ‌yaliyotolewa‌ ‌na‌ ‌Mpango‌ ‌huu‌ ‌ndizo‌ ‌ahadi‌ ‌zangu‌ ‌za‌ ‌uchaguzi‌ ‌kwa‌ ‌wananchi‌ 
ikiwemo‌ ‌kuweka‌ ‌mazingira‌ ‌wezeshi‌ ‌kwa‌ ‌wajasiriamali‌ ‌wadogo‌ ‌ili‌ ‌waweze‌ ‌kufanya‌ ‌kazi‌ ‌zao‌ ‌kwa‌ 
tija‌ ‌”,alisisitiza‌ ‌Mhe.Rais‌ ‌Dkt.‌ ‌Mwinyi‌  
Aliongeza‌ ‌kuwa‌ ‌kujengwa‌ ‌kwa‌ ‌vituo‌ ‌jumuishi‌ ‌vya‌ ‌biashara‌ ‌vipatavyo‌ ‌10‌ ‌visiwani‌ ‌Zanzibar‌ 
kutasadia‌ ‌kuwawezesha‌ ‌wananchi‌ ‌wengi‌ ‌kurasimisha‌ ‌biashara‌ ‌zao‌ ‌na‌ ‌kuondokana‌ ‌na‌ ‌adha‌ ‌ya‌ 
urasimu‌ ‌,‌ ‌hii‌ ‌ikiwa‌ ‌ni‌ ‌moja‌ ‌ya‌ ‌ahadi‌ ‌zake‌ ‌wakati‌ ‌wa‌ ‌uchaguzi‌ ‌mkuu‌ ‌wa‌ ‌mwaka‌ ‌2020.‌ 
Akizungumzia‌ ‌ahadi‌ ‌zake‌ ‌kwa‌ ‌wananchi‌ ‌Mhe.Rais‌ ‌Dkt.‌ ‌Mwinyi‌ ‌amesema‌ ‌kuwa‌ ‌ni‌ ‌pamoja‌ ‌na;‌ 
kuwezesha‌ ‌wananchi‌ ‌kupata‌ ‌mitaji‌ ‌ambapo‌ ‌mpango‌ ‌huo‌ ‌unatoa‌ ‌majibu‌ ‌ya‌ ‌changamoto‌ 
zinazowakabili‌ ‌wananchi‌ ‌katika‌ ‌sekta‌ ‌ya‌ ‌ardhi‌ ‌na‌ ‌biashara‌ ‌kwa‌ ‌kuwaunganisha‌ ‌na‌ ‌Taasisi‌ ‌za‌ 
fedha‌ ‌kupitia‌ ‌hati‌ ‌zao‌ ‌za‌ ‌kumiliki‌ ‌ardhi.‌  
Makamu‌ ‌Mwenyekiti‌ ‌wa‌ ‌Kamati‌ ‌ya‌ ‌Uongozi‌ ‌ya‌ ‌MKURABITA‌ ‌Bi.‌ ‌Immaculata‌ ‌Senje‌ ‌amempongeza‌ 
Mhe.‌ ‌Rais‌ ‌Dkt.Hussein‌ ‌Ali‌ ‌Mwinyi‌ ‌na‌ ‌Mhe.‌ ‌Rais‌ ‌Dkt.‌ ‌John‌ ‌Magufuli‌ ‌kwa‌ ‌kuchaguliwa‌ ‌na‌ ‌wananchi‌ 
kwa‌ ‌kura‌ ‌nyingi.‌  
Aliongeza‌ ‌kuwa‌ ‌MKURABITA‌ ‌imepanga‌ ‌kusajili‌ ‌wajasiriamali‌ ‌1500,‌ ‌kupima‌ ‌viwanja‌ ‌5700‌ ‌katika‌ 
wilaya‌ ‌za‌ ‌Pemba‌ ‌na‌ ‌Unguja,‌ ‌kuendelea‌ ‌kutoa‌ ‌elimu‌ ‌kwa‌ ‌wananchi‌ ‌kuhusu‌ ‌umuhimu‌ ‌wa‌ 
urasimishaji‌ ‌ardhi‌ ‌na‌ ‌Biashara‌ ‌.‌

 

No comments :

Post a Comment