Na Mwandishi Wetu
TAASISI
ya Mico Halal International Bureau imeleta neema mpya kwa walaji wa
nyama ambapo sasa itasimamia machinjio yote nchini kuhakikisha nyama
inayopatikana inakuwa salama kwa afya.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na Katibu wa taasisi hiyo, Shehe Jumanne
Kasonso, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kazi
kwa taasisi hiyo Januari mwaka huu.
Amesema
MICO imepewa kibali na Baraza la Kiislamu Tanzania (Bakwata) kwaajili
ya kusimamia machinjio hayo kwa kupima nyama inayopatikana kuwa safi na
salama kwa matumizi ya binadamu na kutoa vibali kwa wale
wanaozisafirisha nje ya nchi.
Shehe
Kasonso amesema mbali na nyama taasisi hiyo itasimamia pia viwango vya
vyakula na vinywaji kuhakikisha watanzania wanapata huduma yenye ubora
wa hali ya juu na hawapati madhara kiafya.
“Sisi
ni wakala wa Bakwata tunafanya kazi chini yake na mbali na kupima ubora
wa nyama MICO inasimamia na kutoa mafunzo juu ya uchinjaji bora halali
pamoja na kutoa mafunzo na ithibati kwa nyama halali zinazosafirishwa
nje ya nchi,” alisema
Ametaja
baadhi ya wanyama ambao taasisi hiyo imekuwa ikisimamia kuhakikisha
nyama yake inakuwa na ubora na salama kwa matumizi kuwa ni mbuzi,
ng’ombe , kondoo na ndege wanaoliwa.
Shehe
Kasonso amesema taasisi hiyo imenunua mashine maalum na za kisasa
ambazo zitatumika kwaajili ya kupima nyama kwa matumizi ya binadamu ili
kujua kama inamadhara kiafya au la.
“Mtanzania
jali na ipende afya yako hivyo unapotaka huduma ya kupimiwa nyama
wasilianana sisi tuko Magomeni Mapipa jengo la Diamond Trust
tutakuhudumia kuhakikisha unapata nyama ilisayo safi na isiyo na
magonjwa,” amesema Shehe Kasonso
Aidha
ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanakula nyama iliyopimwa isiyo na
magonjwa kama zile ambazo zimechomwa sindano za zandigana na zinginezo
ambazo mnyama husika hatakiwi kuliwa ndani ya siku 30 ili kupisha dawa
hiyo itoke.
“Kuna
dawa ambazo mnyama akichomwa nyama yake haitakiwi kuliwa ndani ya siku
30 na maziwa yake kama anakamuliwa yasinywewe mpaka zipite siku saba
sasa watu wengine wasiowaaminifu wanaweza kuyaingiza sokoni kazi yetu
itakuwa kuyapima kuona kama yanafaa na kama hayafai yanatolewa,”
ameongeza
Amesema
tangu taasisi hiyo ianze kutoa huduma mwezi Januari mwaka huu mwitikio
umekuwa mkubwa kwani watu mbalimbali wamekuwa wakifika kwaaajili ya
kuchukua vibali kutoka MICO kwaajili ya kusafirisha nyama hiyo nje ya
nchi.
No comments :
Post a Comment