Wednesday, February 3, 2021

JKCI YATOA TUZO KWA WAFANYAKAZI BORA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya ngao mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 aliyeshika nafasi ya kwanza Mtoka David Mtoka wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni mbili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 aliyeshika nafasi ya pili Mohamed Songoro wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja na laki tano

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kurugenzi hiyo pamoja na wafanyakazi wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2020/2021. Wapili kushoto ni mfanyakazi aliyeshika nafasi ya kwanza Mtoka David Mtoka aliyetoka katika kurugenzi ya Utawala na Fedha, wapili kulia ni mfanyakazi aliyeshika nafasi ya pili Mohamed Songoro aliyetoka katika kurugenzi ya Utawala na Fedha na katikati ni mfanyakazi aliyeshika nafasi ya tatu Lucas Jilulu aliyetoka katika kitengo cha Ununuzi na Ugavi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 aliyeshika nafasi ya pili Mohamed Songoro wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja na laki tano.


 

No comments :

Post a Comment