Meya wa jiji la
Arusha Maxmillan Iranq’e akiongea na waandishi wa habari katika
maonesho nne ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendelea
mkoani Arusha.
Meya wa jiji la Arusha Maxmillan Iranq’e akiwa katika banda moja wapo lililopo katika mainesho hayo.
Meya wa jiji la Arusha Maxmillan Iranq’e akiwa katika banda la Baraza Ia mifuko ya progaramu za uwezeshaji wananchi kiuchumi
……………………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Jiji la Arusha
limefanya makubaliano ya kukutana na mifuko ya programu za uwezeshaji
wananchi kiuchumi ili kuweza kujenga jukwaa la pamoja la kuwasaidia
wajasiriamali.
Hayo ya yameelezwa na
Mstahiki Meya wa jiji hilo Maximilan Iranq’e wakati akiongea na
waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda katika maonesho ya nne
ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendelea mkoani Arusha.
Alisema kuwa katika
jukwaa hilo watahakikisha kwamba watawavuta wajasiriamali wote wadogo
waliopo mtaani na kuwapa elimu pamoja na mikopo.
“Serikali ina kila
sababu ya kuwasaidia wananchi waweze kuinua uchumi wao ambapo watapa
elimu ya jinsi ya kufanya biashara na kuwapa mikopo Ili kuweza kukuza
uchumi wao na wa taifa kwa ujumla,” Alisema Meya.
Alisema skuwa
serikali inajukumu la kuwalinda wafanyabiashara wake, wajasiriamali na
watu wanaoanzisha viwanda ambapo suala la kuzuia bidhaa za nje
litaaenda taratibu hadi bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zitakapoweza
kukidhi mahitaji.
“Tukisema leo tuzuie
kila kitu kinachotoka nje sidhani Kama hawa wazalishaji wa ndani
wanaweza kutosheleza soko na huwa serikali haikurupuki bali inafanya
utafiti kwanza,” Alieleza.
Aidha alisema kuwa
maonesho hayo ni maonesho yanayohitajika sehemu mbalimbali za nchi kwani
ni sehemu ambapo watanzania wanapata fursa ya kukutana na taasisi za
kifedha pamoja na kujenga mtandao na wafanyabiashara wenzao.
Alisema kuwa
wajasiriamali waliopo katika maonesho hayo ni wajasiriamali wazalendo
wanaozalisha bidhaa kwa kutumia malighafi za ndani hivyo wanahitaji
watanzania wenzao pamoja na serikali kuwaunga mkono.
No comments :
Post a Comment