Belita alisema baada ya kupata fedha za TASAF alichimba shimo na kujnga kisima chenye urefu wa futi 16, kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua ambapo kwa kiwango anachopata pata kwa kila siku anachopata kinamhakikishia kufikisha shilingi milioni 8.1 kwa miezi 9.
Belita alisema kwamba kisima hicho kimekuwa mkombozi kutokana na kumuingizia kipato cha fedha jambo ambalo TASAF imeweza kumsaidia kumuinua kimaisha.
Mlengwa huyo mwenye familia ya watoto 7 ,alisema tangu alipoanza kupata ruzuku hiyo alianza kununua mifugo ya kuku 2. na Mbuzi ndipo alipoweza kuishi vizuri na familia yake.
Aidha Belita aliendelea kusisitiza kwamba amepata mafanikio makubwa kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf,jambo ambalo hakutegemea kufikia hatua hiyo kubwa.
Mlengwa huyo alitaja mafanikio aliyoyapata katika awamu zote ni kulima shamba la mahindi ekari 2 ambapo anategemea kuvuna kiasi cha gunia 45 na kwa sasa amekwisha hifadhi magunia 12 mahindi kwa ajili ya kuuza mara baada ya soko kiwa zuri.
Hata hivyo alisema nje ya mafanikio hayo ameweza pia kujenga nyumba bora na kupangisha wapangaji kwa kila mwezi anawatoza shilingi 20.
Mlengwa huyo alisema ni vema kwa walengwa wanapata ruzuku kupitia mpango huo kutumia wanazopata katika shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kujiua kiuchumi na kuachana na umasikini na wasirudi nyuma .
No comments :
Post a Comment