
MLENGWA wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) Wilayani Igunga Mkoani Tabora Vivian Makala akiendelea jana na
biashara yake uuzaji wa mchele ambao mtaji wake ameuapata baada ya
kupata fedha za ruzuku ya Mfuko wa |Maendeleo ya Jamii(TASAF)
Picha na Tiganya Vincent
……………………………………………………………………………………………………………..
NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA
MLENGWA wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) Wilayani Igunga Mkoani Tabora Vivian Makala amefanikiwa kujenga
nyumba ya kuishi, kusomesha watoto baada ya kupata fedha za ruzuku ya
TASAF na kuanzisha mradi wa kuuza mchele.
Mlengwa huyo alitoa ushuhuda huo
jana wakati ziara ya mfunzo ya viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) na waandishi wa habari walipokuwa kujifunza mafanikio ya
walengwa yaliyotokana na fedha hizo.
Makala alisema baada ya kupata
fedha za TASAF alianza kwa kukunua gunia mmoja ya mpunga na kulikoboa
ambapo alipata kilo 60 alizoziuza kwa shilingi 1,800 kwa kilo na kupata
108,000/= ambazo zilimwezesha kupata mtaji wa kuboresha biashara ya
uuzaji mpunga.
Alisema hatua hiyo
ilimfanya kutumia fedha hizo kumkopesha mkulima wa mpunga aliyezitumia
kulimisha katika mbuga yake na kuzirejesha kwa kumpa gunia 23 baada ya
kuvuna na ndipo hapo mtaji wake uliongezeka.
Makala alisema
kutokana fedha anazopata kutokana na mauzo ya mchele amefanikiwa kununua
eneo na kujenga nyumba ambayo ndio anaishi.
Alisema faiada
nyingine aliyoipata ni pamoja na kusomesha watoto wake kwa kuwapa
mahitaji muhimu kama vile sare, viatu na maftari na kuwa na uhakika wa
watoto wake kula milo mitatu kwa siku.
Makala aliongeza kuwa
fedha anazopata kutokana na mauzo ya mchele zimekuwa pia zikimsaidia
katika matibabu yake ya ugonjwa wa miguu ambao umekuwa ukimsumbua kwa
muda mrefu na kumfanya asiwe na uwezo wa kusimama kwa muda mrefu.
Alisema tatizo hilo
limemfanya kushindwa kujishughulisha na shughuli za shambani na hivyo
kupata mtaji huo kumemsaidia kuweza kupata mahitaji yake ya kila siku.
Mlengwa huyo alisema ni vema kwa walengwa wanapata ruzuku kupitia mpango huo kutumia fedha wanazopewa katika shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kujiua kiuchumi na kuachana na umasikini na wasirudi nyuma .
Mlengwa huyo alisema hata
akitolewa katika Mpango huo hawezi kushindwa kujimudu yeye na familia
yake katika m mahitaji mbalimbali.
No comments :
Post a Comment