Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb)
akiwasili katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini zilizopo
Dodoma, Katika ziara hiyo amelipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa
kuendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo ya kudumisha Usalama wa Raia
na mali zao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb)
akisalimiana na Makamishna wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili katika
ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb)
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro
kuhusu Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini lililopo Dodoma
ambapo ameaidi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Jengo
hilo linakamilika kwa asilimia mia moja ili Watendaji wake waweze
kutekeleza majukumu yao katika mazingira mazuri.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb) akisaini
kwenye kitabu cha wageni katika ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi
(IGP) Simon Sirro Dodoma. Naibu waziri amefanya ziara ya Kikazi katika
Ofisi za makao makuu ya Jeshi laPolisi kujionea namna ya utendaji kazi
wa Jeshi hilo.
No comments :
Post a Comment