Waziri mkuu mstaafu
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Agri Thamani Foundation Mizengo Pinda
akiongea na waandishi wa habari Jana Mara baada ya kufungua mkutano wa
duniani wa kujadiliana jinsi ya kuhamasisha na kuongeza uzalishaji wa
mazao ya mboga hasa yenye asili ya kiafrika inayofanyika jijini hapa
ambapo aliwasisitiza wanahabari kutumia kalama zao kuelimisha wananchi
namna ya kupambana na tatizo la utapia mlo kupitia kilimo cha mboga na
matunda(picha na Woinde Shizza , ARUSHA)
…………………………………………………………………………….
Na Woinde Shizza , Arusha
Kufuatana na takwimu
za Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO) limebaini kuwa
takribani watu milioni 821 wanakabiliwa na matatizo ya utapiamlo
yanayotokana na kula vyakula visichokuwa na viini lishe bora.
Hayo yalibainishwa na
waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa shirika la agri
thamani foundation Mizengo Pinda alipokuwa akifungua mkutano wa
kimataifa unaoangazia mazao ya kiasili ya afrika inayofanyika mkoani
hapa Katika ukumbi wa hotel ya gran melia ambapo alisema kuwa kuwa
upande wa hapa nchini Tanzania Hali ya utapiamlo ni mbaya kulingana na
takwimu za utafiti wa hali lishe ya mwaka 2018 ambazo zinaonyesha
watoto wengi ndio wanaathieriwa sana na tatizo hilo.
Alisema kuwa
kulingana na takwimu hizo zinaonyesha watoto wenye umri kuanzia miaka 0 –
5 milioni tatu wamedumaa,watoto wa miaka 0-5 milioni 1.3 wanauzito
pungufu, watoto wenye umri wa miaka 0-5 milioni tano wanaupungufu wa
Damu ,watoto wenye umri huohuo 0-5 milioni tatu wanaupungufu wa vitamin A
na asilimia 32 ya wanawake wenye umri wa miaka 14 -49 wanatatizo la
uzito uliozidi.
Alibainisha baadhi ya
adhari ya utapia mlo ni pamoja na udumavu ambao una athari Katika
makuzi na maendeleo ya watoto kwa sababu hupunguza ufahamu na ubunifu
kati ya asilimia 30 hadi 40 ambapo hali hiyo huadhiri uwezo wa mtoto
kufundishika ,kuelekezwa na kushusha ufaulu, na pia utapia mlo unaongeza
magonjwa na vifo vya watoto na akina mama.
“Miongoni mwa
asilimia 50 ya magonjwa ambayo husababisha vifo vya watoto wenye umri
Chini ya miaka mitano vinavyosababishwa na utapiamlo ,pia wanawake
takribani 60,000 hufariki kila mwaka kutokana na matatizo ya upungufu wa
damu yanayotokana na tatizo la upungufu wa damu linatokana na upungufu
wa madini china.
Aidha alisema kuwa
mazao ya mboga ni muhimu kwenye afya lishe kwani utafiti wa kitaalam
unaonyesha kuwa mboga za asili ya afrika zina viwango vikubwa vya viini
lishe ukilinganisha na mboga zingine kutoka mataifa ya nje ya bara la
Africa ambapo alibainisha kuwa watu wa nje ya afrika wanayaita mazao
haya kuwa ni “super foods” yaani vyakula venye viini lishe bora kabisa.
“Afrika tunazaidi ya
aina 400 za mazao ya mboga za kiasili lakini yale yanayotumika Kama
chakula ni machache Sana na yale yanayotumika kibiashara ni machache
zaidi ,huu ni urithi wetu wa mazao haya nilazima tuyatunze na kuyaenzi
kwa sababu mbalimbali moja wapo ikiwa mazao ya mboga ni muhimu Sana kwa
afya lishe ,pia kwa ajili ya kutunza bioanuai yetu isipotee
Alisema mbali na
mazao ya mboga kusaidia kupunguza utapia mlo pia ni fursa kubwa Sana ya
kibiashara Katika ngazi ya kaya na taifa kwa ujumla ,kwa afrika na
Tanzania ambapo ukienda sokoni utaona kuwa mboga hizi zimekuwa njia moja
wapo ya kujipatia kipato hasa kwa kina mama na vijana .
“Tanzania Kutambua
ukubwa wa tatizo hili imeamua kupitia ilani ya uchaguzi ya chama tawala
CCM 2020-2025 kuweka uzito mkubwa kwa kuahidi kuhamasisha kilimo cha
mazao lishe Ili kupunguza udumavu kutoka Asilimia 32 hadi 24,pamoja na
kupunguza ukondefu Ili kuendelea kuwa chini ya Asilimia 5 kiwango
ambavyo kimewekwa na dunia, pia kuongeza uzalishaji wa mazao ya bustani
kutoka Tani 7,230,217 hadi tani 14,600,000ifikapo mwaka 2025 na Ili
kufikia malengo haya tuneainisha mambo kadhaa ikiwemo kujengea uwezo wa
taasisi za ndani za serikali na binafsi za ithibati Ili kupunguza
gharama za ithibati za mazao yanayosafirishwa nje hasa mazao ya bustani
na mboga ambavyo wawekezaji wake wakuu ni wanawake na vijana
“alibainisha Pinda
Pinda alisema kuwa
kazi ya kuhamasisha uzalishaji na matumizi ya mazao ya mboga yenye asili
ya kiafrika si kazi ya serikali tu bali ni kazi ya wadau wote wakiwemo
,watafiti ,wakulima,wafanyabiashara na sekta ya usafirishaji,uuzaji wa
mazao ghafi na usindikaji wote wakiungana watafanya kazi nzuri ,aidha
alitoa wito kwa wadau wa Maendeleo wa sekta binafsi na ile ya serikali
kufanya Kila linalowezekana Kuhakikisha mazao haya yanapewa
kipaumbele,pia niasisitize ni vyema tukaweka nguvu nyingi katika utafiti
na hasa Katika maeneo ya ukusanyaji ,utunzaji na uboreshaji wa mbegu za
mazao haya ulimaji bora na matumizi yenye kuimarisha lishe na afya ya
mlaji
Naye mkurugenzi wa
kanda ya mashariki na kusini mwa afrika ,world vegetable center
Dkt.Gabriel Rugalema alisema kuwa mkutano huo utasaidia kuhakikisha
wanajenga mkakati utakao hamasisha ongezeko la mazao haya pamoja na
namna ya kuyatunza
Alisema kuwa zaidi ya
watu 200 wameshiriki moja kwa moja mkutano huu na watu mengine 1000
wameshiriki kwa njia ya mtandao hiyo inatokana na kuwepo na mlipuko wa
Mara yapili ya ugonjwa wa Covid 19.
Naye mchumi wa baraza
la biashara la afrika mashariki (EABC) Adrian Njau aliwataka watu
wajikite kwenye mazao yetu wenyewe kuliko kutegemea mazao ambayo
yanatoka nje ,huku akiwasisitiza wataalam waendelee kufanya utafiti
zaidi wa mboga za ndani.
No comments :
Post a Comment