Tuesday, January 26, 2021

ZAIDI YA BILIONI 8 KUTUMIKA MRADI WA KUONGEZA UZALISHAJI MAJI JIJI LA TANGA


MSIMAMIZI
wa Mradi kutoka Tanga Uwasa Adella Mboya akisisitiza jambo wakati wa
kutoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Kiomoni Jijini Tanga kutambulisha
mradi
huo ambao utakuwa ni wa kuboresha hali upatikanaji wa maji safi katika
Jiji hilo.

 

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Rogers Machaku akizungumza wakati wa mkutano huo
Diwani
wa Kata ya Kiomoni (CCM) Mohamed  Mfundo akieleza jambo wakati wa
mkutano huo ambapo aliishukuru Tanga Uwasa kuwafikia wananchi wake na
kuwapa elimu wa pili kushoto ni Afisa Uhusiano  Msaidizi wa Tanga Uwasa
Anna Makange
AFISA Uhusiano Msaidizi wa Tanga Uwasa Anna Makange akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa kwenye mkutano huo

Afisa
Mtendaji wa Kata ya Kiomoni Adam Harson Chinduka akizungumza

jambo
wakati wa mkutano huo kulia ni Diwani wa Kata ya Kiomoni (CCM) Mohamed
Mfundo na kushoto ni Afisa Uhusiano Msaidizi wa Tanga Uwasa Anna Makange


ZAIDI
ya Bilioni 8 zinatarajiwa kutumika katika mradi mkubwa kuongeza
uzalishaji wa maji Jijini Tanga kutoka lita za ujazo 30 kwa siku  hadi 
kufikia lita 45 kwa siku utakaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga
Uwasa) kupitia wataalamu wake.


Hayo
yalibainishwa leo na Msimamizi wa Mradi kutoka Tanga Uwasa Adela Mboya
wakati wataalamu wa mamlaka hiyo walipokuwa wakitoa elimu kwa wananchi
wa Kata ya Kiomoni Jijini Tanga kutambulisha mradi huo ambao utakuwa ni
wa kuboresha hali upatikanaji wa maji safi katika Jiji hilo.


Alisema
kwamba mradi huo utakuwa ni wa miezi 12 na utakuwa na manufaa makubwa
mawili katika mji wa Tanga la kwanza wananchi upatikanaji wa  maji ya
uhakika ambayo hayakatikikatiki na maji yatapatikana maeneo yote masaa
24.


Alisema
pia wakati wa utekelezaji mradi vijana watanufaika  kwa sababu
watakwenda kuongeza machujio mawili kwenye mtambo wa kusafishia maji
uliopo mowe Pande.


Aidha
alisema hivyo kazi ya ujenzi kubwa itakayofanyika na kuna tenki la
kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita milioni 1 na watakwenda kujenga
jengine lenye ujazo wa lita milioni 1 eneo la Pande .


Alisema
kazi nyengine watalaza bomba kubwa lenye kipenyo cha milimita 600 kwa
urefu wa kilomita 12.5 kutoka mowe mpaka Kange Jeshini na kwenye tenki
hilo bomba litakuwa na kazi ya kusafirisha maji wanayoyazalisha na
watakiwa na mabomba mawili makubwa ya kupelekea maji Tanga.



Hivyo vijana watanufaika kwenye kazi za ujenzi kuchimba mitaro kwani
kwenye mikataba ambayo wataingia na wakandarasi  kwamba kazi yoyote
ambayo haihitaji wataalamu maalumu inatakiwa itoke sehemu ya mradi Kata
ya Kiomoni”Alisema 


Aliongeza
kwamba hivyo vijana wajitokeza kwa wingi kupata hizo  ajira za muda
huku akiwaomba wananchi kuwa tayari kupokea mradi na kutoa ushirikiano
wakati ukitelekezwa kwenye maeneo yao .


“Kutokana
na hilo ndio maana tumepanga kufanya mradi wa  kuongeza miuondombinu ya
kuzalisha maji kutoka mita za ujazo elfu 30 mpaka elfu 45 kwa siku na
mradi huo utaanza mwezi Aprili mwaka huu”Alisema

Awali
akizungumza katika mkutano huo,Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa
wateja Rogers Machaku alisema wanaboresha kwa kiasi kikubwa mtambo wa
Mowe hatua ambayo itasaidia kuongezeka kwa maji yanayozalishwa .


Alisema
pamoja na kuboresha lakini wanachangamoto ya bomba linalotoka Mowe
kwenda mjini eneo la Kange hilo bomba limezidiwa na uwezo hivyo wanataka
kuweka mabomba yawe mawili ambao yote yatakuwa yakipeleka maji mjini.


Naye
kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kiomoni (CCM) Mohamed  Mfundo
aliishukuru Tanga Uwasa kwa kufika kwenye Kata hiyo huku akieleza Kata
hiyo ndio eneo ambalo mamlaka hiyo imewekeza kwa kiasi kikubwa lakini ni
jambo la aibu kwamba baadhi ya maeneo yao hakuna huduma ya maji lakini
kwenye maeneo mengine Jijini humo kuna maji.


Alisema
analizungumza hilo makusudi kwqa sababu mmefika eneo hilo mtaona namna
ya kulifanyia kazi ili kuweza kuondosha changamoto kwenye maeneo ya
Masaini,Mijihoroni,Misufini hayo maeneo kuna watu wanaishi na huduma ya
maji ni ya kwanza.


“Bila
maji hakuna chakula,hakuna mimea,uhai wa chochote hivyo naombeni hizi
changamoto mzichukue muende kuzifanyia kazi hilo ni ombi langu kama
kiongozi wa Kata  mlichukue muone ni namna nani mnaweza kuwapa huduma
maeneo yenye changamoto hizo“Alisema Diwani huyo.

 

No comments :

Post a Comment