Friday, January 8, 2021

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA MHE. WANG YI ATEMBELEA MWALO WA SAMAKI WA CHATO MKOANI GEITA KATIKA SIKU YA PILI YA ZIARA YAKE NCHINI


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Mashimba Ndaki akimpatia maelezo Waziri wa  Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi kuhusu samaki wa aina mbalimbali na minofu yao wanaopatikana katika Ziwa Victoria wakati mgeni huyo alipotembelea Mwalo wa Chato mkoani Geita mapema asubuhi ya leo Ijumaa Januari 8, 2021

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Mashimba Ndaki na Waziri wa  Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi wakipata maelezo kuhusu minofu ya samaki wanaopatikana katika Ziwa Victoria wakati mgeni huyo alipotembelea Mwalo wa Chato mkoani Geita mapema asubuhi ya leo Ijumaa Januari 8,
2021

 Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi akiongea na  wavuvi na wadau wengine wa sekta ya uvuvi alipotembelea na mkujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Mwalo wa  samaki la Chato Mkoani Geita alikotembelea leo Ijumaa Januari 8, 2021 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akimkaribisha rasmi nchini Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi na ujumbe wake kabla ya kufanyika mazungumzo rasmi wa pande hizo mbili mjini Chato mkoa wa Geita  leo Ijumaa Januari 8, 2021 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake nchini

PICHA NA IKULU

 

No comments :

Post a Comment