Wednesday, January 27, 2021

Wananchi wafurika banda la NHIF Wiki ya Sheria Dodoma

Afisa Matekelezo wa NHIF Amandus Machal akiwapa maelezo kuhusiana Mfuko unavyofanya kazi katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Catherine Kameka akiwahudumia wananchi waliofika katika Banda la NHIF kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.

Baadhi ya wananchi wakipata taarifa ya Mfuko huo katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika Viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.

*******************************************

*NHIF yaahidi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi

Na Ripota Wetu ,Michuzi Tv

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema kuwa katika kulinda afya ni kuwa na

Bima ya Afya ambayo itafanya kuwa na uhakika wa matibabu bila ya kuwa na fedha.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika Viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma Afisa Uhusiano wa NHIF Catherine Kameka amesema wananchi watumie fursa ya maadhimisho hayo kupata elimu na mrejesho wa taarifa mbalimbali kuhusu Mfuko.

Amesema kuwa Mfuko uko kwa ajili ya kuwahudumia watanzania ili kuwa na uhakika wa matibabu.

Aidha amesema kuna aina mbalimbali za kujiunga na Mfuko kutokana na mtu anavyohitaji na vyote vinafanya kazi.

Kameka amesema kuwa mwitikio ni mkubwa kwa wananchi kujiunga na Mfuko na kupata elimu namna Mfuko unavyofanya kazi.

Amesema Serikali nia yake ni kuona wananchi wake hawapati changamoto za matibabu ndio maana ikaweka mfuko huo huku Serikali ya awamu ya Tano inayokwenda kasi katika uchumi ikitaka kulinda rasilimali watu yenye afya.

 

No comments :

Post a Comment