Katika hafla hiyo Naibu Waziri Ulega alivitaka vyama na Mashirikisho ya michezo kuwa wawazi na wawajibikaji katika matumizi ya fedha za wadhamini ili kuwapa imani wadau wengi zaidi kuwekeza na kudhamini michezo.
Aidha, ametoa rai kwa CRDB Bank kudhamini mashindano yajayo ya michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA ili kusaidia katika kuibua vipaji vya vijana shuleni.
Pia, Naibu Waziri Ulega ametoa wito kwa wawekezaji na makampuni mbalimbali kusaidia katika ujenzi wa miundombinu ya michezo hapa nchini kupitia fedha za Corporate Social Responsibility - CSR ili vijana wengi waweze kunufaika.
Kupitia udhamini huo, CRDB wamewapatia wanamichezo 25 takribani shilingi milioni 50 kwa ajili ya kugharamia masomo katika vyuo mbalimbali hapa nchini.
No comments :
Post a Comment