Wednesday, January 27, 2021

UFUNGAJI WA KIKAO KAZI KATI YA SERIKALI NA MASHIRIKAYASIYO YA KISERIKALI NCHINI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Tanzania Bara wakati wa kikao kazi kati ya Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilichofanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akitoa maelezo kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na NGOs wakati wa kikao kazi kati ya Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilichofanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Neema Lugangikira akizungumza katika kikao kazi kati ya Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilichofanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatila hotuba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel wakati wa kikao kazi kati ya Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilichofanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

…………………………………………………………………………………

Na Mwandishi Maalum

Serikali imesema iko tayari kuendelea kupokea maoni kuyafanyia kazi kama ambavyo imekuwa

ikifanya na kuendeleza ushirikiano katika maeneo yote ambayo Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanafanya kazi katika kuleta maendeleo na ustawi wa nchi yetu.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel wakati akifunga kikao Kazi cha siku mbli kati ya Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika sekta na nyanja mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma za kijamii, utawala bora, uchumi na maendeleo ya watu kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

“Nimefarijika kuambiwa kwamba, hoja nyingi zilizotolewa zimejibiwa kikamilifu na kutolewa ufafanuzi na watendaji wa Serikali waliopo hapa. Ni matumaini yangu kwamba kikao hiki kimetuwezesha kuelimishana, kujadiliana na kubadilishana uzoefu katika utendaji wa majukumu ya kila mmoja wetu katika kuimarisha uendeshaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali” alisisitiza

Amesisitiza kuwa kila mmoja akitimiza wajibu wake kikamilifu sekta hii ina uwezo wa kutoa mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya nchi yetu na ametoa wito Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kutumia kikao kazi hicho kuwa kiwe chachu ya kuleta mabadiliko katika kutekeleza majukumu yao.

Aidha Dkt. Mollel amezitaka NGOs kuweka nguvu kwenye uwekezaji wa shughuli za kiuchumi ili kupata rasilimali za kuendesha shughuli mnazofanya. Napenda niwatie moyo na kuwahimiza kutekeleza azma hii, kwani jambo hili likifanyika kama mlivyopanga litaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na mchango wake katika maendeleo ya Nchi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewashauri wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuhakikisha wanashirikiana na kutoa taarifa kwa Serikali kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili mchango wao uweze kuonekana katika ujenzi wa taifa.

Naye Mwakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Neema Lugangira ameowaomba wadau wenzake wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutumia fursa ya kuwa na mwakilishi katika Bunge ili kuifanya Sekta ya NGOs.

Awali akisoma taarifa ya Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Kaimu Mkurugenzi wa ACTII Rehema Tukai amesema Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yataendelea kukishirikia katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo kwa wananchi katika maneneo amabayo Serikali haijayafikia.

 

No comments :

Post a Comment