***************************************************
Na Woinde Shizza ARUSHA
Kamishna mkuu wa
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Dkt Edwin Mhede amesema kuwa mamlaka
hiyo haiongezi muda wa wafanyabiasha kuboresha mashine za EFD badala
yake itachukua hatua za kisheria kwa ambao bado hawajaboresha.
Dkt Mhede aliyasema
hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa nusu mwaka wa mamlaka hiyo ambapo
alipokea dodoso la kuombwa kuongezwa muda wa wafanyabiasha kuboresha
mashine za EFD .
Alisema kuwa jambo
la kuongeza muda haliwezekani kwani zoezi hilo linaweza kufanyika kwa
muda mfupi na walipewa muda wa kutosha kuanzia Desemba 7, 2020 hadi
Januari 7,2021.
Alieleza kuwa ombi
hilo amelikataa na wafanyabiashara wote ambao bado wachukuliwe hatua
kwani wakianza kutengeneza mazingira ya kuongeza muda watakuwa wanacheza
na hawatafikia lengo la uboreshaji huo.
“Suala la EFD mashine
zenye protocol 2.1 sio chagua la mfanyabiashara bali ni lazima kila
mfanyabiashara awe amefanya maboresho haya maboresho ni lazima
yaendane na aina ya mashine tunazozitumia hivi sasa na upatikanaji wake
ni wa dakika chache kwahiyo nasema kuongeza muda ni jambo ambalo
haliwezekani inajulikana wazi kuwa utiifu wakati mwingine lazima watu
walazimishwe,” Alisema Dkt Mhede.
Alifafanua kuwa kama
upatikanaji EFD hauzidi masaa mawili au matatu na waliwapa mwezi mzima
ni kwanini waongeze muda, ambapo aliagiza baada ya kutoka katika
mkutano huo wakachukue hatua kwani hawatakuwa na namna nyingine zaidi ya
kwenda kuwapa motisha watii kwa mujibu wa sheria lakini suala la
kuongeza muda hicho kitu hakitakuwepo.
Naye naibu kamishina
wa mamlaka ya mapato Tanzania ,(TRA) Msafiri Mbibo alisema kuwa mkutano
huu utasaidia kuweza kujua namna ya kutatua matatizo yaliopo katika
sekta yao ,pamoja na kupanua mikakati itakayo saidia kupata mapato
mengi yatakayo wezesha kufikia malengo waliojiwekea.
Alibainisha kuwa kazi ya taasisi hii ni kuweza kusaidia serikali kujenga taifa linalojiweza kiuchumi pamoja na kimaendeleo.
Aliongeza kuwa
mkutano huu utasaidia kuwawezesha kujadili njia bora itakayosababisha
utendaji kazi kuwa mzuri ,ambapo pia watajadili namna ya kutatua
matatizo waliyonayo ikiwemo upungufu wa idadi ya Wataalam wa mamlaka
hiyo , upungufu wa vitendea kazi pamoja na ukosefu wa nyumba za
Wataalam wanaoishi maeneo ya mipakani.
No comments :
Post a Comment