Sunday, January 10, 2021

TPDC YAFANYA TATHMINI YA KINA YA ATHARI ZA KIMAZINGIRA UTAFITI WA MAFUTA

Timu ya Wataalam kutoka TPDC ikiwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu kujadiliana na wadau wa masula ya mazingira kwa lengo la kufanya utafiti wa kina wa kimazingira kabla  ya kuanza hatua ya juu ya zaidi ya utafiti wa mafuta Kishapu Shinyanga.

Timu ya Wataalam kutoka TPDC ikiongozwa na Dkt. Allan Mzengi katikati ambaye ni Mshauri mwelekezi na kushoto kwake ni Bw. Abraham Maeda ambaye naye mtaalam mshauri pamoja na Bw. Gaston Kanuti Mjiolojia kutoka TPDC ikiwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu kujadiliana na wadau wa masula ya mazingira kwa lengo la kufanya utafiti wa kina wa kimazingira kabla ya kuanza hatua ya juu ya zaidi ya utafiti wa mafuta Kishapu Shinyanga.Viongozi wa Kata pamoja na watendaji wa kata ya Masanga iliyoko Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ikisikiliza kwa makini timu ya wataalam kutoka TPDC waliofika katika kata hiyo kutoa Elimu ya utafiti kuhusu hatua za utafiti wa mafuta itakayofanyika katika kata hiyo hivi karibuni.

***************************************************

Na Anthony Ishengoma-Shinyanga.

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) inafanya tathimini ya kina ya athari za

kimazingira katika mikoa mitano ya Tanzania ambayo inaguswa na utafiti wa mafuta unaoendelea hivi sasa katika mikoa hiyo ambayo kwa pamoja iko katika bonde la mto Manonga, Wembele na Ziwa Eyasi.

Kwasasa Shirika hilo liko katika Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kukutana na wadau pamoja na wananchi walioko katika vijiji vya eneo la mradi kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi ili kujiweka tayari kupokea wataalam watakaofanya tathimini hiyo lakini pia kupata ufahamu wa ujenzi wa mikuza zoezi litakalo fuata baada ya kukamilisha tathimini ya kimazingira.

Akiongea na  viongozi wakata na vijiji ambavyo tathimini hiyo itafanyika katika Wilaya Kishapu Mtaalam Mwelekezi wa Mradi huo wa utafiti wa Mafuta Dkt. Allan Mzengi alisema utafiti huo umefikia katika hatua ya kushirikisha wadau walioko katika eneo la mradi kwa kuwa ni muhimu kwa viongozi na wananchi kufahamu umuhimu wa mradi huo.

Dkt. Mzengi aliongeza kuwa TPDC iko katika hatua muhimu ya kufanya tathimini ya kimazingira ili kubaini shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo na namna gani zainavyoweza kuathiriwa na shughuli za utafiti na hatimaye kushirikiana na jamii husika kupata muhafaka kwa manufaa ya maendeleo ya utafiti wa mafuta.

Naye mtaalam wa Jiololijia kutoka Shirika la TPDC Bw. Gaston Kanuti aliongeza kuwa shirika hilo litakapokamilisha hatua muhimu ya kutathimini shughuli za mazingira itawasilisha ripoti ya matokeo ya utafiti huo katika Baraza la Mazingira NEMC ili iweze kujiridhisha na kutoa cheti kitachowezesha TPDC kuendelea na hatua muhimu ya uchorongaji wa Mikuza.

Aidha Bw. Kanuti amewataka wananchi watakao kuwa katika eneo la mradi kutokuwa na wasiwasi kwa kuwa baada ya utafiti wa data za mitetemo kukamilika ardhi itakayokuwa imetumika itarudishwa kwa mwenyewe na ikigundulika eneo husika litachimbwa kisima cha mafuta kama yatapatikana mhusika atalipwa fidia.

Aidha Bw. Kanuti alifafanua kuwa ucorongaji wa njia za mikuza utawezesha watafiti kuweka vilipuzi ardhini vitakavyolipuliwa kwa lengo la kubaini mitego ya mafuta na vilipuzi hivyo vitaweka kama inavyooneshwa katika ramani inayoonesha ramani ya eneo la utafiti.

Pamoja na ufafanuzi wa mtaalam wa jiolojia kutoka TPDC Mtaalam mshauri kutoka Kampuni ya MTL Consulting Bw. Abraham Maeda aliwambia viongozi hao wa vijiji kuwa utafiti huo wa athari za kimazingira utaangazia pia masuala ya mambo kale akiyataja kuwa ni kama maeneo ya makaburi na matambiko kwani ikitokea maeneo kama hayo yanachangamoto mkuza unaweza kupindishwa kwa lengo la kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Bw. Maeda aliongeza kuwa utafiti wa athari za kimazingira unafanyika kwa kuzingatia matakwa ya kisheria akiitaja ya sheria ya mafuta ya mwaka 2015 na sheria ya mazingira ya mwaka 2005 ambazo zinaelekeza ni nini kifanyike kabla ya kuendelea na utafiti mkubwa kama huu.

Utafiti huu unafanyika kufuatia hatua ya awali ya utafiti huu iliyohusisha utafiti wa kutumia ndege uliotumuika ili kubaini aina ya miamba iliyoko katika Bonde la Eyasi Wembele uliobaini uwepo wa miamba yenye sifa za kuzalisha mafuta katika Bonde hili la mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida, Simiyu na Manyara na Arusha.

 

No comments :

Post a Comment