Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki,akizungumza na waandishi wa habari Ofisini
kwake wakati akitoa taarifa juu ya mlipuko wa ugonjwa wa homa ya Nguruwe
kwenye baadhi ya wilaya za mikoa ya kanda ya ziwa Januari 23,2021
jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mifugo
kutoka wizara ya mifugo na Uvuvi Prof.Herzon Nonga akitoa ufafanuzi juu
ya mlipuko wa ugonjwa wa homa ya Nguruwe kwenye baadhi ya wilaya za
mikoa ya kanda ya ziwa Januari 23,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imepiga
marufuku wananchi wa kanda ya ziwa kula nyama ya nguruwe ikiwa ni hatua
za kukabiliana na mlipuko wa homa ya nguruwe uliotokea hivi karibuni.
Aidha imewaagiza
wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi kuhakikisha wanasimamia kikamilifu
karantini zilizowekwa kwaajili ya kutibu nguruwe ambao tayari
wameathirika na ugonjwa huo.
Akizungumza na
waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dodoma Januari 23,2021 Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki alisema taarifa zilizopo
zinaonyesha homa ya nguruwe ilianzia kwenye halmashauri 6 ya kanda ya
ziwa.
“Kutokana na uwepo wa
homa ya Nguruwe tumewataka wananchi wa kanda ya ziwa kuacha kula nyama
ya nguruwe ilikukabiliana na ugonjwa huu hatari ambao hauna tiba wala
kinga,
” Nawaagiza viongozi
mnaohusika mikoani na wilayani kuhakikisha mnasiamia karantini
zilizowekwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa ugonjwa huu hausambai kwenda
maeneo mengine na kuleta madhara”alisema
Mhe. Ndaki alizitaja
halmashauri ambazo hazitaruhusiwa kula nyama ya nguruwe kuwa ni
Mbogwe,Sengerema,Geita,Misungwi,Kyerwa na kahama ambazo kwa kiasi
kikubwa zimeathilika na ugonjwa huo.
Alisema hadi kufikia
januari 22 mwaka huu zaidi ya nguruwe 1500 sawa na asilimia 10 ya
nguruwe wote nchini wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
“Serikali inaendelea
kufuatilia na kufanya kila linalowezekana kuhakikisha ugonjwa huu
unadhibitiwa haraka iwezekanavyo iliusienee katika maeneo mengine na
kusababisha hasara kwa wafugaji wengi zaidi” alieleza
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Mifugo Prof.Ezron Nonga alisema lengo la kuzuia wananchi
kula nyama ya nguruwe ambayo imeathirika na ugonjwa huo ni kudhibiti
usienee kwa kasi katika maeneo mengine ambayo bado hayajaathilika
Aliwataka wafugaji
wahakikishe wanatoa taarifa za ugonjwa au vifo vya nguruwe Mara
vinapotokea, na pindi wanapokufa kuhakikisha wanazikwa kwa kuchimba
shimo refu au kutekezwa kwa moto
“Ugonjwa wa homa ya
nguruwe huanzia kwa nguruwe pori na baadaye husambaa kwa nguruwe wa
kufugwa kwa njia ya kugusana,damu,mate,kinyesi na maji maji mengine
yanayotoka kwa wanyama wagonjwa au kugusa vifaa vyenye maambukizi”
alieleza
No comments :
Post a Comment