Muonekano
wa jengo la maabara katika kituo cha Utafiti wa malisho ya Mifugo
TALIRI-Tanga ambalo limejengwa kwa ruzuku kuutoka Serikalini kupitia
COSTECH
Banda linalotumiwa na kituo cha TALIRI Tanga kwenye utafiti wa kuku.
Mzani
wa kisasa wa kidijitaliunaotumika kupima uzito wa wanyama katika Kituo
cha Utafiti TALIRI-Tanga ambao umejengwa kwa ruzuku kutoka Serikalini
kupitia COSTECHKITUO
cha Utafiti wa Mifugo Tanga kilicho chini ya Taasisi ya Utafiti wa
Mifugo (TALIRI) kilianzishwa miaka ya 1950 kikiwa na jukumu la kufanya
utafiti wa malisho ya mifugo katika Kanda ya Mashariki inayojumuisha
mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Taasisi
hii ni kongwe na imekuwa na changamoto ya uchakavu wa majengo pamoja na
miundombinu ya kufanya utafiti hivyo kupelekea kuwepo kwa uhitaji wa
ukarabati na ujenzi wa majengo mapya ili kufanikisha utoaji wa huduma
bora kwa wananchi.
Aidha,
kutokana na mahitaji hayo kituo kiliomba Ruzuku kutoka Serikalini
kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili kufanya
maboresho ya maabara, jengo la kufundishia kwa vitendo ufugaji kuku wa
kisasa, chumba cha kupozea pamoja na mizani ya kisasa ya kidijitali ya
wanyama.
Ufungaji
wa mizani ya kidijitali upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji,
mfumo huu utakapokamilika utawezesha kutambua uzito wa mfugo ambao ni
muhimu sana kwa kila mfugaji, daktari wa mifugo hata watafiti. Kipimo
hiki husaidia kutambua maendeleo ya afya ya mfugo husika, kuandaa
chakula kinachoendana nayo, kukadilia dozi ya dawa pindi mfugo ukiugua
hata kukadilia kiwango cha mazoezi anayohitaji kwa ajili ya uzalishaji
wenye tija.
Ruzuku
iliyotelewa na Serikali kupitia COSTECH imesaidia taasisi hiyo katika
utekelezaji wa miradi hivyo kwani imekiwezesha kituo kudhibiti ubora wa
mazao ya mifugo na malisho kwa mikoa ya kanda ya pwani.
Mradi
huu unaojumuisha miundombinu mitatu ni muhimu kwa kwa unaleta tija kwa
wadau wa sekta ya mifugo kuanzia taasisi yenyewe, wafanyakazi wake,
wakulima, wazalishaji na waagizaji wa chanjo.
No comments :
Post a Comment