Saturday, January 30, 2021

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KATIKA MIJI YA TABORA, IGUNGA NA NZEGA PIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA JENGO LA IDARA YA WAGONJWA WA HUDUMA YA DHARURA HOSPITALI YA KITETE MKOANI TABORA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati akikagua ujenzi wa Matanki makubwa ya kuhifadhia maji katika mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati akikagua ujenzi wa Matanki makubwa ya kuhifadhia maji katika mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akizindua mradi mkubwa wa Maji ya Ziwa Victoria itakayo hudumia miji ya Tabora, Igunga na Nzega.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati akitoka kukagua ujenzi wa Matanki makubwa ya kuhifadhia maji katika mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Huduma ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Huduma ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua ujenzi wa jengo la Huduma ya Wagonjwa wa Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021. PICHA NA IKULU

 

No comments :

Post a Comment