Thursday, January 28, 2021

RAIS DKT.MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA CHAPULWA KAHAMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Chapulwa Kahama mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Kiwanda cha Nafaka, Vinywaji na Maziwa (Kom Limited) Kahama mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mawaziri, pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Shinyanga akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Kiwanda cha Nafaka, Vinywaji na Maziwa (Kom Limited) Kahama mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Januari 2021. Kiwanda hicho kinatarajiwa kuanza kufanya kazi Mwezi Julai mwaka huu.

Baadhi ya viongozi mbalimbali pamoja na wabunge wakipiga makofi mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza kumsamehe Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Mji wa Kahama Anderson David Msumba (aliyesimama)ambaye alikuwa miongoni mwa Wakurugenzi wachache walionunua Magari ya Kifahari tofauti na maagizo ya Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telak ili aweze kumsaidia Mama Cristina Masigwa ambaye anadai kudhulumiwa kipande cha Ardhi mkoani Shinyanga.

Mama Cristina Masigwa akizungumza kuhusu kero yake ya kudhulumiwa kipande cha Ardhi mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu. PICHA NA IKULU

 

No comments :

Post a Comment