Monday, January 25, 2021

RAIS DK.JOHN MAGUFULI ASAMEHE WAFUNGWA 1,789 AMBAO NI RAIA WA ETHIOPIA,KUREJESHWA KWAO WAKATI WOWOTE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari wa mkoa wa Geita mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.

 Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS Dk.John Magufuli ametangaza kutoa msamaha kwa wafungwa 1789 ambao ni raia wa

kutoka nchini Ethiopia ambao wamehukumiwa vifungo kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

Dk.Magufuli ametoa msamaha huo leo Januari 25, mwaka 2021 akiwa Wilayani Chato mkoani Geita alipokuwa akizungumza mbele ya Rais wa Ethiopia Mhe. Sahle -Work Zewde ...ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Akifafanua kuhusu wafungwa kuwapa msamaha,Rais Magufuli amesema wafungwa hao walihukumiwa vifungo kutokana na kuingia nchini kinyume cha sheria na wote hao 1789 waliingia nchini bila kufuata utaratibu.

"Tumezungumza na Mheshimiwa Rais wa Ethiopia namna ya kupanga mbinu za kuwaruhusu warejee kwako na nimemueleza kwa kutoa ahadi ya kutokuwa na masharti ya aina yoyote, nimewaruhusu waondoke free.Nimefanya hivyo kwa kuzingatia udugu na urafiki kati nchi yetu na Ethiopia.

"Na nimemueleza mheshimiwa Rais kuwa wanandege kule za Shirika la Ndege la Ethiopia Airline ,wakichukua Dreamliner inayobeba watu 260 wakienda mara tano watakuwa wamechukua wafungwa wengi tu.Kati ya hawa wafungwa ambao tumewasemehe wapo waliokaaa gerezani kwa zaidi ya miaka saba,"amesema Rais Magufuli.

Hivyo watakaporejea nchini kwao watakwenda kushiriki kikamilifu kujenga uchumi wa nchi yao ya Ethiopia na kwamba Rais..amekubali atakaporejea nchini kwake atakwenda kujadiliana na na wenzake namna ya kuwarejesha raia hao."Mimi nimewaruhusu hata leo wakiweza wawachukue bila masharti yoyote."

Aidha Rais Magufuli amesema.mbali ya kuzungumzia wafungwa hao, wamezungumza mambo mengine mbalimbali yanayohusu nchi hizo na kubwa zaidi ni kuendelea kujenga uchumi huku akieleza kufurahishwa kwake na ujio wa Rais huyo kwani ni heshima kubwa kwa nchi yetu.

Hata hivyo amemwambia kwamba "Nchi kwetu tunalokabila la Wairak ambao kihistoria wanatokea nchini Ethiopia na miongoni mwao yumo aliyekuwa Waziri Mkuu Frederick Sumaye lakini hii ndiyo uafrica wetu, ndio undugu.

"Lakini pia nimemueza ombi letu dogo kwenye uwanja wetu kule Ethiopia kwasababu tulichelewa kujenga ofisi za ubalozi wetu,tulipeleka fedha zikaliwa ,hivyo tumechelewa kujenga na sheria ya kule ukipewa kiwanja na ukachalewa kujenga unanyang'anywa.Hivyo tulinyang'anywa na sasa tunaomba tena ili tujenge, Rais amekubali ombi letu na atalishughulikia atakaporudi nyumbani,"amesema Rais Magufuli.

Pia amemueleza Rais huyo kwamba na wamepewa kiwanja cha ukubwa wa heka tano ili wajenge ofisi za ubalozi wao nchini Tanzania.

No comments :

Post a Comment