****************************************
Na Woinde Shizza ,ARUSHA
Jeshi la Polisi nchini limewafukuza kazi kwa fedheha askari wake wanne kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu ,rushwa na wizi.Akiongea na vyombo
vya habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha ,Salumu Hamduni alisema kuwa
askari hao wametimuliwa kazi jana januari 6,Mwaka huu .
Alisema kabla ya
kufukuzwa kazi kwa askari hao ,walifikishwa kwenye mahakama ya kijeshi
na kukutwa na hatia na kwamba watafikishwa mahakamani Kama vibaka
wengine wanaojihusisha na matukio ya uhalifu.
“Askari hao
tumewafukuza kazi baada ya kuwafikisha kwenye mahakama ya kijeshi na
watashtakiwa Kama vibaka wengine wa kawaida”alisema Kamanda
Aliwataja askari hao
kuwa ni pamoja na askari mwenye namba G. 5134 DC Heavenlight Mushi
aliyekuwa Askari kitengo Cha Intelijensia Mkoa wa kipolisi kinondoni
jijini Dar es Salaam,H.125 PC Gasper Paul kitengo Cha Intelijensia makao
makuu Dodoma na H.1021 PC Bryton Murumbe aliyekuwa askari wa kawaida
mkoani Dodoma.
Kamanda alifafanua
kwamba askari hao wamefukuzwa kazi kutokana kwa kosa la kumteka
mfanyabiashara wa Madini jijini Arusha,Sammy Mollel ambaye ni mkurugenzi
wa kampuni ya madini ya Germs and Rocks Venture ya jiji Arusha na
kujipatia kiasi cha sh, milioni 10 kinyume cha sheria.
Alisema askari hao
wakikamatwa desemba 24,2020 katika ofisi za mfanyabiashara huyo baada ya
kufika kwa ajili ya kuchukua mgao wa pili wa shilingi milioni 20 kati
ya milioni 30 walizohitaji na kupatiwa sh,milioni 10.
Mwingine aliyefukuzwa
kazi ni askari mwenye namba F.1445 CPL Koplo William Joseph mkazi wa
Muriet jiji Arusha ambaye alikamatwa jana nyumbani kwake akiwa na na
bidhaa mbalimbali haramu ikiwemo misokoto ya bangi.
Alisema kuwa askari
huyo alikutwa na misokoto 20 ya bangi bhangi kwenye gari lake
,kukiunganishia umeme wa wizi kinyume cha sheria,kupatikana na pombe ya
gongo lita tano na lita mafuta ya Dizel Lita 85.
Pia alikutwa na vyuma
vya bomba kinyume na taratibu,pombe ya viroba boksi 84 iliyookatazwa na
serikali,chupa 9 za konyagi na pakti 3 za pombe aina ya kiroba .
Kamanda alisema kuwa
upelelezi wa matukio hayo umekamilika na majalada yamepelekwa ofisi ya
taifa ya mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi na majalada hayo yakirudi
watafikishwa mahakamani
No comments :
Post a Comment