Monday, January 18, 2021

NAIBU WAZIRI KIPANGA ATOA WITO KAMATI YA USIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI WA CHUO CHA VETA KOROGWE KUHAKIKISHA UNAKAMILIKA KWA WAKATI


Naibu Waziri
wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga akisisistiza jambo  wakati wa ziara
yake ya siku moja ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Veta wilayani Korigwe mkoani
Tanga mradi unaojengwa chini ya Usimamizi wa Chuo cha Veta Kihonda mkoani
Morogroro wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa wa
kwanza kushoto (aliyevaa tisheti nyeupe) ni Mkuu wa Chuo cha Veta
Kihonda Morogoro na Msimamizi wa Mradi huo Maganga Kashinde

Naibu Waziri
wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga akisisistiza jambo  wakati wa ziara
yake ya siku moja ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Veta wilayani Korigwe mkoani
Tanga mradi unaojengwa chini ya Usimamizi wa Chuo cha Veta Kihonda mkoani
Morogroro wa pili kulia Mkuu wa Chuo cha Veta
Kihonda Morogoro na Msimamizi wa Mradi huo Maganga Kashinde

Naibu
Waziri
wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga katikati akikagua ujenzi wa
chuo cha Veta wilayani Korogwe wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa

Muonekano wa ujenzi wa baadhi ya majengo ya Chuo cha Veta wilayanu Korogwe

Fundi akiendelea na ujenzi kwenye Chuo cha Veta wilayani Korogwe kama alivyokutwa

Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga amefanya
ziara ya kutembelea Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi

(VETA)
wilayani Korogwe Mkoani Tanga huku akitoa wito kwa kamati inayosimamia
mradi wa ujenzi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati uliopangwa.

Akiwa
katika katika ziara ya kukagua mradi huo ambao unasimamiwa na chuo cha
VETA Kihonda cha mkoani Morogoro alionesha kuridhishwa na hatua
iliyofikiwa na kushauri matumizi ya jeshi la akiba kama vibarua ili
kuharakisha utekelezaji wa mradi huo.

Kipanga alisema kwamba
amekagua mradi huo na kuridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa hadi
sasa na kuwaagiza wasimamizi wa mradi kuhakikisha unakamilika kwa wakati
uliopangwa ikiwemo kuwashauri kutumia vibarua kutoka Jeshi la Akiba kwa
kuwa wapo wengi ambao wanaweza kufanya kazi hizo.

Hata hivyo
Naibu Waziri huyo alitoa wito kwa wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha
vifaa vya upauaji vinapatikana mapema ili ujenzi uweze kukamilika kwa
muda uliopangwa.

“Kwa kuwa majengo karibu yote yamefikia hatua
ya upauaji, nitoe rai kuwa vifaa vya upauaji vipatikane mapema ili
ujenzi uendelee na kukamilika kwa wakati,” amesisitiza Mhe. Kipanga.

Awali
Akisoma taarifa ya ujenzi wa chuo hicho, Mkuu wa chuo cha VETA Kihonda,
Kashindye Maganga amesema ujenzi wa mradi huo unagharimu kiasi cha
Bilioni 1.6 huku kiasi ambacho walikwisha kupokea ni Tsh.Milioni 940.2
na hadi sasa wametumia kiasi cha Tsh.Milioni 917.9 na kiasi kilichobakia
ni milioni 22.2 hivyo fedha ambazo imetumika ni sawa na asilimia 57.37
ya fdha ya mradi wote.

Alisema mpaka sasa mradi huo umefikia 34
ya kazi zote na kazi iliyobakia kwa sasa ni kumalizia kufunga
lenta,kupaua na kazi ya umaliziaji ambapo tayari walikwisha kuomba fedha
kwa ajili ya kumalizia kazi hizo na wanategemea kukamilisha kazi ya
mradi huo ifikapo Machi 31 mwaka huu endapo fedha walizoomba watapatiwa
mapema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa
akizungumza katika ziara hiyo alionyeshwa kufurahishwa na hatua ya
Serikali kujenga chuo hicho katika Wilaya yao na kwamba anaamini chuo
hicho kikikamilika kitatoa vijana mahiri watakaotumika kiuzalishaji
katika viwanda mbalimbali nchini .

 

Mkuu
huyo wa wilaya aliahidi kushirikiana na Kamati ya ujenzi kuhakikisha
vijana wa jeshi la akiba wanapatikana haraka ili kuweza kukamilisha
ujenzi huo kwa wakati uliopangwa.

 

No comments :

Post a Comment