Thursday, January 14, 2021

NAIBU WAZIRI KASEKENYA AIPONGEZA TANROADS KWA MABADILIKO YA KIUCHUMI

……………………………………………………………………………………………..

Na Mwandisi Wetu

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya amesema Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), wana mchango mkubwa katika mabadiliko ya

kiuchumi yanayoendelea kufanyika nchini.

Mhandisi Kasekenya ameyasema hayo alipotembelea ofisi za TANROADS kwa lengo la kufahamiana na wafanyakazi na kupata taarifa za utendaji za Wakala.

AmesemaTANROADS ambao wako chini ya wizara yake, wanafanya kazi nzuri za kuhakikisha miundombinu ya barabara, madaraja, viwanja vya ndege inatengenezwa na kupitika wakati wote.

Naibu Waziri amewapongeza  TANROADS kwa kuacha kufanya kazi kwa karatasi au kwa kuamini, badala yake sasa wanafanya kazi kielektroniki.

Amesema alipokwenda kwenye chumba cha CCTV, ameweza kuona jinsi maofisa wa eneo la mizani wanavyoweza kufuatilia kituo chochote cha mizani na kuona vitu vinavyoendelea.

“Pale mizani unaweza kupata taarifa ya gari lolote unalolitaka kwenye vituo ambavyo tayari vimeunganishwa,” amesema Naibu Waziri Kasekenya.

Amesema kuwa, kazi kubwa ya mizani ni kulinda barabara, kwani itachangia kupunguza ajali na kusaidia vyombo kutojaza mzigo zaidi ya kipimo halisi.

Naibu Waziri ameutaka Wakala wa Barabara kuliangalia na kulipatia ufumbuzi suala la watu kufanya kazi za kibinadamu ndani ya hifadhi za barabara.

“Hasa barabara hizi za changarawe, suala la kufanya kazi za kibinadamu ndani ya hifadhi ya barabara ni la kawaida sana, mfano barabara ya kutoka Mpanda kwenda Kalema, imebaki kama tuta,” amesema Naibu Waziri na kuiagiza TANROADS kutoa elimu ya kutosha ili kuhakikisha watu hawaingilii hifadhi za barabara kwa shughuli za kibinadamu.

 

No comments :

Post a Comment