Naibu Waziri Kilimo Hussein Bashe akiwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Simiyu Bwana Enock Jacob na Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu Bi. Miriam Mmbaga wakifuatilia mkutanpo wa Wadau wa pamba uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Bariadi, Simiyu leo tarehe 17 Januari, 2021.
Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini Bwana Marco Mtunga akitoa taarifa ya maendeleo ya tasnia ya zao la pamba leo kwenye mkutano wa Wadau wa zao la pamba katika ukumbi wa mikutano wa Bariadi, mkoani Simiyu leo tarehe 17 Januari, 2021.
Wakuu wa mikoa inayolima pamba nchini kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye Mkuu wa mkoa wa Singida Rehema Nchimbi pamoja Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima wakifuatilia mkutano wa Wadau wa zao la pamba katika ukumbi wa mikutano wa Bariadi, mkoani Simiyu.
Dkt. Benson Ndiege Mrajis Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika akiwa pamoja na Wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano wa Wadau wa zao la pamba.
Naibu Waziri Kilimo Hussein bashe akiwahutubia Wadau na Washiriki wa mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa Bariadi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri Kilimo Hussein bashe akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba wakishuhudia Mwenyekiti wa Nyanza Cooperative Union (1984) Ltd Bwana Benjamin Mikomangwa akitia saini mkataba wa kuongeza tija na uzalishaji (Performance Agreement) kati ya Bodi ya Pamba, Vyama vya Ushirika na Vyama vya Msingi vya Mazao (AMCOS) na Tume ya Maendeleo ya Ushirika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Bariadi mkoani Simiyu.
……………………………………………………………………………………..
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (Jana) tarehe 17 Januari, 2021 ameongoza tukio la
kihistoria la utiaji saini mkataba wa kuongeza tija na uzalishaji (Performance Agreement) wa zao la pamba mwaka 2021 kati ya Bodi ya Pamba, Vyama vya Ushirika na Tume ya Maendeleo ya Ushirika.Awali Waziri Bashe amesema tija ya sasa kwa Wakulima wengi wa zao la pamba katika mikoa mingi ni kilo 200 wakati tija inapaswa kufikia angalau kilo 800 kwa heka.
Mkataba huo umejikita katika makubaliano ya matumizi ya pembejeo za pamba za msimu wa pamba wa 2020/2021.
“Zao la pamba ni kila kitu kwa Wakulima wa mikoa ya Kanda ya Ziwa; zao la pamba ni miongoni mwa mazao ya kimkakati katika Awamu ya Tano. Uzalishaji wenye tija katika zao la pamba unahitaji upatikanaji wa pembejeo mbalimbali ikiwemo mbegu, mbolea na viuadudu”. Amekaririwa Naibu Waziri Bashe.
Lengo la mkataba huo ni kuhakikisha pembejeo zinapatikana na zinasambazwa kwa Wakulima kwa wakati kupitia mfumo wa ushirika na zinatumika ipasavyo ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao la pamba kwa msimu wa 2021.
Naibu Waziri Bashe amesema Serikali imeazimia kuongeza uzalishaji wa zao la pamba kwa kuhamasisha matumizi sahihi ya pembejeo na hivyo kutoa maelekezo kwa Bodi ya Pamba, Vyama Vikuu na Vyama vya Msingi (AMCOS) kuingia makubalaiano ya matumizi sahihi ya pembejo za pamba kwa msimu wa 2021.
“Wakulima wa zao la pamba watasambaziwa pembejeo kwa kuzingatia uzalishaji na mahitaji ya pembejo husika kupitia Vyama vyao vya Msingi (AMCOS)”.
Naibu Waziri Bashe amesema Wakulima watasambaziwa pembejeo kupitia AMCOS zao kwa kuzingatia makadirio ya uzalishaji na idadi ya Wakulima kwa mchanganuo wa aina ya mbolea (Mbegu/Mbolea na Viuadudu kwa kiasi cha idadi ya mbegu, mbolea na ujazo wa viuadudu husika. Kati ya Bodi ya Pamba na Vyama Vikuu na Vyama Vikuu na Vyama vya Ushirika vya Mazao (AMCOS).
Aidha; Naibu Waziri Bashe amesema kupitia tani elfu 12 (12,588) za mbegu bora zilizosambazwa kwa Wakulima nchi nzima; Matarajio ya kitaifa ni kuzalisha pamba tani laki 5 kwa nchi nzima kwa msimu wa kilimo wa 2021.
“Uzalishaji wetu kwa mwaka huu usipungue tani laki 5(500,000) nchi nzima. Ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anafanya kwa sehumu yake na inawezekana kabisa kuzalisha hadi tani milioni 1”. Amemalizia Naibu Waziri Bashe.
No comments :
Post a Comment