Sunday, January 3, 2021

MWENYEKITI UVCCM TAIFA AWATEMBELEA WASTAAFU WA UVCCM ZANZIBAR







MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Komred Kheri James amewatembelea

viongozi wakuu wastaafu wa UVCCM Mjini  Zanzibar hii leo.

komred kheri amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndg Seif khatibu,Ndg Hamadi Masauni,na Ndg Sadifa juma Khamisi.

Akiwa Katika ziara hiyo kwa nyakati tofauti leo, komrade kheri James amesema kuwa UVCCM Taifa inatambua mchango wa viongozi hao katika ujenzi wa Umoja huo na wataendelea kuwa pamoja katika kushauriana na hasa katika ujenzi wa Jumuiya na Chama.

"UVCCM Taifa inatambua kazi zilizotekelezwa na Viongozi hawa wakati wa Uongozi wao sisi Vijana tunajifunza kwao kwani uwepo wao kwetu sisi ni hazina, tutaendelea kuimarisha mahusiano ili tuendelee kujifunza mambo mazuri kutoka kwao kwa ustawi wa Umoja wetu’’ amesema James. 

Aidha kwa nyakati tofauti Viongozi hao wamepongeza Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chini ya Mwenyekiti wake Komred Kheri James kwa uimara na kuimarisha Umoja na Mshikamano kwa Bara na Visiwani.

Pia Viongozi hao wameupongeza Umoja wa wa Vijana kwa kuwa sehemu ya Ushindi wa Chama Cha mapinduzi katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Komred kheri yuko Visiwani zanzibar kwa majukumu ya maandalizi ya uzinduzi wa  matembezi ya mapinduzi Siku ya tarehe 5/01/2021 kuelekea Siku ya kilele cha Sherehe za mapinduzi ya Zanzibar.

 

No comments :

Post a Comment