Sunday, January 31, 2021

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WFC) WATOA ELIMU YA FIDIA KWA POLISI MKOA WA ARUSHA

Meneja wa Mipango na Utafiti wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),Patrick Ngwila akizungumza wakati wa semina kwa askari polisi mkoa wa Arusha kuhusu mfuko huo na namna polisi wanavyoweza kushirikiana na mfuko huo kuwapa haki wafanyakazi baada ya kupata majanga.

Afisa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Arusha,Abass Mcharo akizungumza wakati wa semina kwa  polisi mkoa wa Arusha iliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) namna polisi na mfuko wanaweza kushirikiana katika kuwapa haki wafanyakazi baada ya kupata majanga.

Afisa Madai wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),Gladness Mandembwe akiwasilisha mada wakati wa semina hiyo iliyofanyika kwenye Bwalo la Polisi mkoa wa Arusha.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Wilbroad Mutafungwa akizungumza na maafisa wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) baada ya semina kwa polisi mkoa wa Arusha.

Baadhi ya askari Polisi waliohudhuria semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

 

No comments :

Post a Comment