Friday, January 8, 2021

Mbunge wa Kibamba awapatia zawadi wagonjwa Mloganzila.


Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji  Dkt. Deogratias Manyama akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzilaa  mara baada ya kupokea zawadi hizo Mbunge wa jimbo la Kibamba Mhe. Issa Mtemvu akizungumza na baadhi ya viongozi na waandishi wa habari mara baada ya kuwapatia zawadi wagonjwa hospitalini hapa.

Mhe.Issa Mtemvu akimkabidi Bw. Zablon Mchagula zawadi wakati alipotembelea wodi ya wanaume hospitalini hapa (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji Dkt. Manyama.Mtemvu akimpa pole Bw.Abduly Rashid alipokuja kutembelea wagonjwa Mloganzila.

************************************************

Mbunge wa jimbo la Kibamba  Mhe.Issa Mtemvu  amewatembelea wagonjwa katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na kutoa    zawadi kwa  baadhi ya wagonjwa wenye uhitaji .

Zawadi hizo zimejuisha pampasi za watu wazima, mafuta ya nazi,Maji ya kunywa,sabuni,miswaki  pamoja na dawa ya meno

Akipokea zawadi hizo kwa niaba ya Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Deogratias Manyama amemshukuru mbunge huyo kwa kuwatembelea wagonjwa na kutumia fursa hiyo kueleza baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali ikiwemo gharama za uendeshaji pamoja na changamoto ya vyombo vya usafiri.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi katika wodi ya wagonjwa wenye uhitaji hospitalini hapa,  Mhe. Issa Mtemvu amesema kuwa lengo la kutembelea Mloganzila ni kutoa mkono wa pole kwa wagonjwa na kuwatakia heri ya mwaka mpya.

 “Nimekuja kuwapa mkono pole kama mwakilishi wenu bungeni na kuwatakia heri ya mwaka mpya pamoja na kutumia fursa hii kusikiliza changamoto zinazoikabili hospitali hii ili niweze kuziwasilisha bungeni kwa waziri mwenye dhamana”amesema Mhe. Mtemvu

Mhe. Mtemvu amewataka wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ambayo itawasaidia kupata matibabu kwa uhakika.

 

No comments :

Post a Comment