MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA MKUU WA JKT CHARLES MBUGE KATIKA SKIMU YA UMWAGILIAJI YA KIKOSI CHA CHITA JKT 837
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge akifurahia
jambo na Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa wanaojenga miundombinu ya
Skimu ya umwagiliaji ya Kikosi cha Chita JKT 837 uliopo Ifakara Mkoani
Morogoro.
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge akiangalia
jinsi maji yanavyopita katika moja ya banio ambalo litatumika kugawa
Maji kwenda katika mashamba ya mpunga katika mradi wa umwagilkiaji
unaojengwa na kikosi cha 837 Chita JKT Ifakara,Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja General Charles Mbuge
akitembelea moja ya ghala embalo litatumika kuhifadhia mpunga
utakaovunwa katika mashamba hayo ya kimkakati wakati alipofanya ziara
kuangalia maendeleo ya mradi huo uliopo Ifakara Mkoani Morogoro.:Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge akiangalia moja ya mfereji wa kupeleka maji unaojengwa katika skimu ya umwagiliaji ya Chita JKT kikosi 837 Chita JKT, unaopita chini ya reli unaopeleka maji katika mashamba ya mpunga wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya mradi huo Ifakara Mkoani Morogoro.Ujenzi wa miundombinu ya skimu hiyo umefikia asilimia 45 na unategemea kukamilika mwezi Mei 2021.Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Meja General Charles Mbuge
akiangalia sehemu ya ekari 2500 zilizopandwa mpunga na kikosi cha 837
Chita JKT wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya mradi huo uliopo Ifakara mkoani Morogoro.Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge akiangalia moja ya mfereji wa kupeleka maji unaojengwa katika skimu ya umwagiliaji ya Chita JKT kikosi 837 Chita JKT, unaopita chini ya reli unaopeleka maji katika mashamba ya mpunga wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya mradi huo Ifakara Mkoani Morogoro.Ujenzi wa miundombinu ya skimu hiyo umefikia asilimia 45 na unategemea kukamilika mwezi Mei 2021.
No comments :
Post a Comment