Wednesday, January 27, 2021

MASHINE YA UPIMAJI KIAMBATA HAI CHA DAWA YAWA MSAADA MKUBWA MAABARA


Mchunguzi wa Dawa wa TMDA Kanda ya Ziwa  Kapilya Haruni akionesha waandishi Habari namna mashine inavyofanya kazi katika kutambua Kiambata katika dawa wakati waandishi walipotembelea Maabara hiyo jijini Mwanza.


* Yafafanua unywaji dawa  wa maji baridi au Moto pamoja na maziwa 

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa imeweka imekuwa

na mashine mbalimbali  lengo ni kuhakikisha Dawa zinadhibitiwa katika kulinda afya za wananchi .

Moja ya mashine katika Maabara ya TMDA Kanda ya Ziwa ni 'Distller Solution' ambayo ina kazi kubwa katika kupima  kiambata hai  cha dawa ili mtumiaji anayotumia iweze kutibu ugonjwa husika.

Mashine hiyo ina  mfumo wa tumbo la Binadamu  ambapo ndio inaweza kutambua dawa inavyoweza kufanya kazi mara baada ya kupata kiambata.

Akizungumza na waandishi wa Habari Katika Maabara ya Kanda ya Ziwa ya Mamlaka hiyo Mchunguzi wa Dawa Kapilya Haruni amesema dawa ili iweze kufanya kazi ni lazima ichunguzwe kiambata chake kilichomo katika kibebeo na ndipo kujiridhisha kuingia sokoni kwani bila kufanya hivyo kuna uwezekano baadhi ya wafanyabiashara wakaingiza dawa ambazo hazina kiambata na madhara yake watu wanaweza kutumia dawa na wasiweze kupona.

Amesema mashine hiyo ni umuhimu mkubwa katika kufanya uchunguzi wa dawa kwa kupima uzito pamoja na kiambata katika kulinganisha na viwango vilivyowekwa vya dawa husika kwenye kiambata.

Haruni amesema kuwa mashine hiyo ina matumbo nane ambayo yote hufanya kazi kwa kuangalia na kujiridhisha kwa kila tumbo kama viwango vyake viko sawa kwenye uchunguzi wa  dawa kwa kujua kiambata.

Aidha amesema kuwa mashine hiyo wakipima na kujiridhisha dawa ambayo imeletwa haina uhalisia viambata kwa viwango vilivyowekwa wanapeleka katika ngazi maamuzi ya kufanya dawa isisajiliwe.

Haruni amesema dawa zote zinapimwa kabla hazijapata usajili ikiwa na lengo la kulinda watumiaji wasipate madhara yatokanayo na Dawa.

Amesema kuwa katika utumiaji wa dawa hakuna tatizo la kutumia maji ya baridi ,Moto kwani kinachotafutwa kwenye dawa ni kiambata ambacho ndio kinakwenda kufanya kazi huku kuna baadhi ya Dawa unaweza ukanywa na maziwa katika kusaidia dawa kufanya kazi.

Hata hivyo amesema  dawa zina viwango vilivyowekwa ambapo wenyewe ni kupima katika mazingira yote ya dawa ikiwemo na mazingira.

 

No comments :

Post a Comment