Saturday, January 9, 2021

Malengo muhimu mstaafu mtarajiwa kujipangia 2021

 Retired Santa Rosa Junior College administrator Greg Granderson was one of the few black faculty members during his 25-year  tenure. Photo taken on Monday, Sept. 21, 2020.  (John Burgess / The Press Democrat)

Inatakiwa kama mstaafumtarajiwa iwe umeshaanza kuandaa mpango wako wa kustaafu mapema, na kama bado hujaanza kujipanga kwa ajili ya kustaafu, ni bora ukaanza sasa. (Picha ya Mtandaoni)

Na Christian Gaya:

Majira Ijumaa 08 Januari 2021

Kama msataafumtarajiwa inatakiwa uhakikishe ya kwamba, unaandaa mpango mtandao wa kuwa na ushirikiano wa kitaaluma na kila mtu unayekutana naye wakati upo kazini, na pia hakikisha mara kwa mara unaongeza mtandao wako kwa kuwa karibu nao zaidi, ili kuongeza umuhimu wako kwenye fani yako na pia kujijenga kikazi.

Inatakiwa ujenge sifa zako kwa kuhakikisha kuwa, unatekeleza ahadi na majukumu yako kwa wakati muda uliopangiwa.

Pia, inatakiwa ujenga urafiki wa kweli na kuwa karibu na watu hao kwa kukwepa kuwa na mtandao wa kimyakimya na usiokuwa na faida yoyote, na hata vilevile inatakiwa  utanue mtandao wako kwa kutoka nje ya taaluma yako zaidi.

Watu hao baadaye huenda wakawa ni hazina na msaada mkubwa kwako wakati ikitokea umepunguzwa kazini.

Usitoe akili yako yote ya kazi mia kwa mia kwa mwajiri wako, sababu inapaswa kujiuliza iwapo hali halisi ya kazi yako kila siku haina changamoto mbaya yoyote?

Wewe kila siku ni kuamuka na kujiandaa kwenda kazini, na kufanya kazi kwa masaa nane ikiwemo saa ya muda wa kula  chakula mfano mchana, baada ya hapo huwa ni kurudi nyumbani na kujikalia kwenye kochi, pengine na kutazama vipinndi vya luninga ‘televisheni’, ama  kwenda kwenye vitivirefu mpaka inapofika muda wa kulala.

Na mtindo wa mzunguko wa maisha yako ya namna hiyo unaendelea hivyo hivyo mpaka leo?

Kama hii ndiyo ratiba yako, basi tuseme uko kwenye kampuni inayokufaa sana?

Basi kampuni yako, basi tuseme uko kwenye kampuni inayokufaa sana, na kampuni yako inakupa saa nzuri za uzalishaji kutokana na wewe mwenyewe kuitumikia ipasavyo.

Hata hivyo, hiyo pia maana yake ni kwamba, badala ya saa zako ambazo ungetumia kwa ajili ya kujiendeleza wewe mwenyewe, unayatumia muda wako kizembe unavyojua mwenyewe.

Kwa nini usiweze kuwekeza muda wa siku yako baada ya saa za kazi, kwa kujifunza kupata ujuzi fulani kwa kuhudhuria darasani upya, hata kwa kujisomea vitabu ya kujiendeleza wewe mwenyewe, kwa kutumia hata wasifa wako kwenye shirika au kampuni mbalimbali?!

inatakiwa ujiongeza, na hasa kujiongeza zaidi kwenye sehemu ulizobobea, kwa kujisomea au kwa kuchukua kozi zinazohusiana na taaluma yako, na hata kutawanya uwezo wako zaidi.

Jifunze ujuzi na mbinu mpya za kazi, kwa kuchukua kozi mpya na kuendelea kujifunza zaidi na zaidi.

Hakuna mtu ambaye yeye ni wa muhimu zaidi kuliko mwenzake kwa ajili ya maisha yako, lakini na wewe pia unaweza kubadilika na kuwa mwenye thamani kubwa katika kampuni na kama hata ukiachishwa kazi, bado ukawa unavutia kuajiriwa kwenye taasisi nyingine tena, inachotakiwa ni kujiendeleza wewe mwenyewe. 

Inatakiwa uwe umeanza kuandaa mpango wako wa kustaafu tayari, kama hujaanza kupanga kwa ajili ya kustaafu, ni bora ukaanza sasa mapema.

Kuna msemo unaosema ya kuwa inaonesha Watanzania wengi mara nyingi wamekutwa hawana maaandalizi ya mpango wowote wa kustaafu.

Takwimu za karibuni zinatisha. Chukulia kama watanzania 100 ambao kwa sasa wana umri wa miaka 45, kwa muda watakapofikia umri wa miaka 60 wa kustaafu, inawezekana wakalazimika waendelee kufanya kazi au kuwa mizigo itakayoendelea kutegemea familia zao kuendesha maisha yao.

Asilimia ndogo sana, huenda ndio maisha yao yatakuwa mazuri, na asilimia moja tu huenda itakuwa wanafurahia maisha yao baada ya kustaafu.

Vijana watasema kustaafu itachukua muda mrefu sana kwao kufikia huko. Kitu ambacho bado hatujagundua ni kwamba hatujui ya kuwa kila siku ya Mungu tunazidi kuzeeka.

Hivyo jaribu kuanzisha biashara yako ndogo kwa ajili ya kujipatia pato la ziada.

Kwa kufanya hivi itakusaidia wakati siku utakapopoteza ajira yako.

Unahitaji kufanya utafiti, na lengo mojawapo iwe ni kupata biashara ambayo unaweza kuendesha kulingana na wewe unachokipendelea na uwezo wako uliokuwa nao.

Na kuhakikisha ya kuwa haingilii na kuathiri kazi yako uliyoajiriwa nayo.

Unapoanza kuifanya mapema ndiyo vizuri zaidi, kwa sababu huitaji kukimbizanakimbizana, na hiyo hukupa nafasi ya kufanya makosa na kurekebisha vizuri zaidi.

Pia inaweza kuwa vizuri zaidi kuanza biashara yako kwa kutumia kifurushi chako cha kustaafu.

Watu wenye maarifa ya kitaaluma mbalimbali wanaweza kujifikiria kuwa washauri, ambapo gharama zao za kuanzia kutoa ushauri si kubwa ukilinganisha na gharama za kuanzishia biashara.

Inatakiwa kujisomea na kujifunza kuhusiana na somo hili la fedha na pensheni mara kwa mara.

Maisha kuhusu kukua na kuongezeka, na hivyo kufanya kila siku kuwa na mahitaji ya kutumia fedha kwa ajili ya kupata mahitaji muhimu.

Lakini fedha ni kitu kinachoweza kutuletea fedheha, na kisichoeleweka, na wakati mwingine na humfanya mtu kuwa mtumwa, badala ya fedha kuwa mtumwa wako.

Hivyo ni kitu cha kutumia kwa uangalifu sana katika maisha yetu ya kila siku ili kukwepa dhihaka inayoweza kukubadili siku zijazo.

Na njia kuu ya kukuza fedha, ni kujiongezea fedha kwa elimu yako ya fedha na ya pensheni.

Na kuhakikisha kuwa unawekeza kwa kufuata kanuni za usalama wa mtaji, uwezo wa kuleta faida, uwezo wa kitega uchumi chako kubadilika kuwa fedha taslimu, na kutawanya uwekezaji wake.

Na njia kuu ya kukuza fedha ni kwa kupanua elimu yako ya fedha na ya pensheni. Na kuhakikisha ya kuwa unawekeza kwa kufuata kanuni za usalama wa mtaji, uwezo wa kuleta faida, uwezo wa kitega uchumi kubadilika kuwa fedha taslimu, na kutawanya uwekezaji.

Kwa kujiongezea elimu ili kujiongezea yanayohusiana na mitaji ya fedha, itakuwezesha kuwa na matumizi mazuri katika maisha yako, na kuisha bila msongo wa maisha.

Ni muhimu sana kujitambua kuhusu ujinga wako uliokuwa nao kuhusiana na fedha, kwa sababu  mtajikihatarishiki sana wakati unapotaka kuzitunza na kuziongeza zaidi.

Kumbuka pia kuwa, mara nyingi fedha hutokana na mawazo ya mtu anayowaza.

Christian Gaya ni mwanzilishi wa Kituo cha HakiPensheni, mshauri na mtaalamu wa masuala ya pensheni na kustaafu. Kwa maelezo zaidi: gayagmc@yahoo.com +255 655 13 13 41, unaweza kutembelea www.hakipensheni.blogspot.com, info@hakipensheni.co.tz

 

No comments :

Post a Comment