Monday, January 25, 2021

MAKUNGU AELEZA FURSA LUKUKI ZA UWEKEZAJI MKOANI TABORA

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(wa saba kutoka kushoto
mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Kijeshi
kutoka Nchi mbalimbali kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC)
walikuwa katika ziara ya kimafunzo Mkoani Tabora hivi karibuni

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (aliyesimama)
akizungumza na Maafisa wa Kijeshi kutoka Nchi mbalimbali kutoka Chuo
cha Taifa cha Ulinzi (NDC) walikuwa katika ziara ya kimafunzo Mkoani
Tabora hivi karibuni.

WAWEKEZAJI toka ndani na nje ya Tanzania wametakiwa kujitokeza
kuwekeza Mkoani Tabora kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali kutokana
na mazingira kuwa rafiki kwa shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora
Msalika Makungu kwa Maafisa wa Kijeshi kutoka Nchi mbalimbali kutoka
Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) walikuwa katika ziara ya kimafunzo
Mkoani Tabora hivi karibuni

Alisema kuwa maeneo mbalimbali ambayo yanafaa kwa uwekezaji mdogo na mkubwa.

Makungua alisema asilimia 50 ya ardhi yote inayofaa kwa kilimo bado
haijatumika katika shughuli za uzalishaji na hivyo kwa wawekezaji
wahitaji wanakaribishwa.

Alitaja mazao yanayokuwabali mkoani humo ni pamoja na mazao ya nafaka,
aina ya mikunde, mazao ya mizizi na matunda kama vile miembe.

Mazao mengine ya biashara ambayo hukubali Mkoani humo ni pamba na tumbaku na hivi sasa mkoa huo unaendelea mkakati wa kulima korosho katika
mashamba makubwa.

Alisema katika kuhakikisha kuwa wanabadilisha kilimo cha Mkoa huo na
kuwa cha kisasa wameanza kuandaa kilimo cha mashamba makubwa ya
korosho katika eneo la Karangasi wilayani Uyui na wanatarajia kuwa na
aina ya mashamba hayo katika maeneo ya Halmashauri mbalimbali za Mkoa
huo.

Makungu alisema Mkoa huo una maeneo makubwa yanayofaa kwa kilimo cha
umwagiliaji kwa ajili ya uzalishaji wa mpunga na mazao mengine.

Alisema katika kudhibitisha hilo kuna mradi mkubwa wa umwagiliaji wa
Mwamapuli uliopo wilayani Igunga umeonyesha mafanikio makubwa ambao
uzalishaji wake umesababisha kuibuka kwa viwanda vya kati vya kukoboa
na kuchambua mchele ambao unasafirishwa katika Nchi mbalimbli.

 Makungu alisema wanaendelea na mkakati wa uboreshaji wa
mifugo hasa Ng'ombe wa asili ili kuwawezesha Wafugaji kuongeza kipato
badala ya kuendelea na ufugaji wa mazoea ambao kuwa na Ng'ombe wengi
wasiokuwa na tija kwao.

Alisema nje ya mkakati huo tayari wamepata mbegu kutoka Wizara ya
Mifugo kwa ajili ya kuhamilisha ng’ombe wa asili ili kupata koosafu
bora.

Makungu alisema lengo ni kutaka wafugaji Mkoani Tabora kuachana na
ufugaji wa kimazoea wa kuona ufahari wa kuwa na kundi kubwa la ng’ombe
ambao hawana tija na kuingia wa na ng’ombe wachache wanaotikana na
kosafu bora.

Alisema kuna fursa za kuwekeza katika sekta ya Utalii kutokana na
uwepo Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla ambayo inaweza kuvutia utalii wa
uvuvi na kuangalia wanyama wa aina mbalimbali waliomo katika Hifadhi
hiyo.

Makungu aliongeza kuwa mbalimbali utalii pia zipo shughuli za
uchimbaji madini katika Wilya ya Sikonge , Igunga na Nzega.

Katibu Tawala huyo wa Mkoa alisema uwepo wa mistu asili mikubwa
inaweka mazingira mazuri ya ufuagaji wa nyuki wa kisasa na uanzishwaji
wa viwanda vidogo na vikubwa vya kuchakata asali kwa ajili ya
kuiongezea thamani.

 

No comments :

Post a Comment