Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amefanya Ziara katika Idara ya
Watu wenye ulemavu , Idara ambayo ipo chini ya ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Lengo la ziara hio ni kukutana na watendaji wa Ofisi, kujua Changamoto zao na kubadilishana mawazo.
Mkurugenzi
wa Idara hio Bi.Abeda Rashid Abdallah amesema miongoni mwa majukumu yao
Idara ni kusimamia upatikanaji wa haki na usawa kwa watu wenye ulemavu
pamoja na kusaidia na kusimamia Mikataba ya watu wenye ulemavu.
Bi.
Abeda amesema mpaka kufikia sasa Idara yao imeshafika mpaka ngazi ya
shehia na nahii ni kwaajili ya kusaidia utambuzi wa watu wenye ulemavu
katika ngazi za mitaa na matatizo yao ili kuweza kuwasaidia.
Mkurugenzi
Abeda amesema kwasasa wanapigania kujua idadi ya walemavu wote, wanatoa
elimu ya Uzazi kwa watu wenye ulemavu pamoja na kutoa misaada ya vifaa.
Akifafanua
katika hilo amesema; ‘’Database yetu Jumuishi inaonesha mpaka sasa
tuna Wananchi 8330 ambao wana ulemavu, lakini tuna zaidi ya walemavu
1267 Zanzibar ambao tayari tumeshawapatia vifaa mbalimbali kama vile
viti vya walemavu, magongo na hata lotion kwaajili ya walemavu wa
ngozi’’.
Akielezea Changamoto zao Mkurugenzi amesema katika
majengo mengi ya taasisi sio rafiki kwa walemavu jambo ambalo
linawafanya walemavu kushindwa kuzifikia huduma.
Mkurugenzi Abeda
amesema Idara ina mfuko wa watu wenye ulemavu ambao hutumia pia
kukopeshana na mpaka sasa walemavu 85 wameshanufaika na mfuko huo ila
changamoto ni kwamba ni wagumu wa kurudisha fedha hizo nakudai ni mali
ya serikali hivyo zinafaa kuwanufaisha wao nasio kuzirejesha.
Akimalizia
Mkurugenzi amesema wapo baadhi ya walemavu ambao wanaombaomba
mabarabarani jambo ambalo sio zuri kwani tayari walishawafikia na
kuwataka wafike ofisini kujiorodhesha nakuona namna yakuwasaidia lakini
imebainika upo mtandao wa watu hao kutumika kuomba ikiwa ni kama ajira
na kuwanufaisha watu wengine ambao wanawafadhili.
Mkuu wa Wilaya
ya Mjini Unguja Mh. Rashid Simai Msaraka amesema yeye yupo tayari
kushirikiana na Idara ya watu wenye ulemavu pamoja na kusaidiana katika
kutatua kesi za uzalilishaji zinazowakuta, hivyo muda wowote
watakapomuhitaji wasisite kuwasiliana nae.
Makamu wa kwanza wa
Rais Maalim Seif amesema jamii haipaswi kuwadharau wala kuwatenga
walemavu kwani yoyote kati yetu ni mlemavu mtarajiwa.
Maalim
amesisitiza kwa kusema; ‘’Katiba yetu ya Zanzibar inakataa ubaguzi wa
aina yoyote ile, hivyo nikosa kuwabagua walemavu, Walemavu wanastahiki
kuheshimiwa nakupewa haki zao zote’’.
Maalim amesema pia
inahitajika elimu kwa jamii juu ya ulemavu kwani wapo wanaodhani kuzaa
mtoto mwenye ulemavu ni mikosi au laana hivyo kupelekea kuwaficha watoto
hao na kuwakosesha haki zao za msingi katika jamii kama raia.
Makamu
ameeleza kwamba ipo haja ya majengo yote ya biashara au yakutoa huduma
yoyote yawape vipaombele Walemavu katika kujenga miundo mbinu ya
kuwasaidia nao kufikia huduma hizo.
Maalim amemuagiza Mkuu wa
Wilaya ya Mjini Mh. Msaraka kuwadhibiti wale wote wanaowatumia walemavu
kuomba pesa mabarabarani kwaajili ya kuwanufaisha wao na kuwafanya kama
kitega uchumi.
Maalim amesisitiza kwamba zipo taarifa kuna watu
wanawachukua walemavu na kuwaleta Zanzibar, Maalim amesema kwamba
hakatazwi mgeni kuja Zanzibar ila sio kuja kuombaomba, hivyo ni
kuwadhalilisha walemavu na jambo hilo halipaswi kuvumiliwa.
Maalim
amemalizia kwa kusema wapo walemavu ambao wanashiriki michezo ya
kitaifa au kimataifa nakurudi na medali nyumbani hivyo ipo haja Serikali
kuwaita, kuwatambua na kuwapa moyo.
No comments :
Post a Comment