Maafisa utamaduni
kutoka Kanda ya kaskazini wakiwa katika picha ya pamoja wakati
wakiendelea na kikao kilichoandaliwa na Basata jijini Arusha(Happy
Lazaro)
…………………………………………………………………..
Happy Lazaro,Arusha
Arusha.Baraza la Sanaa la Taifa limewataka
wasanii wote nchini kuhakikisha wanafanya shughuli zao kwa kufuata
sheria ,taratibu na kanuni na kuepuka ukwiukaji wa maadili .
Hayo yalisema Jana na
Mratibu wa shughuli za Sanaa Kanda ya kaskazini,Flora Mgonja wakati
akizungumza katika kikao Cha maendeleo ya sekta ya sanaa Kanda ya
kaskazini kilichoandaliwa na Basata na kuwashirikisha maafisa utamaduni
kutoka Kanda ya kaskazini.
Mgonja alisema
kuwa,lengo la mkutano huo ni kuweza kukutana na kujadili namna ya
kuboresha utendaji kazi katika Sanaa ili waweze kushirikiana kwa pamoja
katika kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa ili kusimamia maadili.
Alisema kuwa,Basata
hawapo kwa lengo la kuwafungia wasanii bali kuweka utaratibu kwa ajili
ya kazi zinazofanyika kuhakikisha inafuata utaratibu pasipo kuwepo kwa
ukwiukaji wowote wa sheria.
Alisema kuwa,
taratibu na sheria za Basata zinamtaka kila msanii kuweza kusajiliwa na
akitoa kazi yake yoyote bila kusajiliwa atachukuliwa hatua za kisheria
,hivyo kuwataka kufuata taratibu hizo ili kazi zao ziweze kufanyika kwa
weledi mkubwa.
Naye Katibu Mkuu wa
umoja wa wanamuziki Tanzania,Stella Joel alisema kuwa,uwepo wa semina
hiyo utasaidia sana kuwakumbusha utendaji kazi wasanii hao kwa
kushirikiana na maafisa utamaduni na kuweza kufuata sheria na kanuni za
kazi zao.
“kwa kweli semina hii
inasaidia sana kutukumbusha wajibu wetu katika utendaji kazi huku
tukisimamia maadili ya wasanii,na italeta manufaa makubwa Sana kwani ni
njia mojawapo ya kuongeza ushirikiano wa karibu Kati ya wasanii na
maafisa utamaduni katika kufuata maadili.”alisema Stella.
Naye Afisa utamaduni
jiji la Arusha, Elizabeth Ncheye alipongeza viongozi wa Basata kwa
kuwakutanisha maafisa utamaduni katika kujadiliana namna ya kufanya kazi
kwa pamoja katika kushirikiana na kuhakikisha maadili yanafuatwa katika
wasanii.
Alisema kuwa,kwa
kuwakutanisha pamoja kunaongeza ufanisi na tija katika utendaji kazi
katika kuhakikisha kwa pamoja wanasimamia maadili na kuweza kuondokana
na changamoto mbalimbali zinazowakabili wasanii katika utendaji kazi
wao.
Kwa upande wake
,Afisa utamaduni jiji la Tanga ,Rose Sempoli alisema kuwa,uwepo wa kikao
hicho unawasaidia Sana kuwakumbusha wajibu wao katika utendaji kazi wa
kila siku na kuhakikisha sheria na taratibu pamoja na maadili yanafuatwa
katika kazi za wasanii .
No comments :
Post a Comment