Friday, January 29, 2021

KUSAYA ATAKA MAAFISA KILIMO NA WADAU WA UGANI KUWEKA MIKAKATI YA KUPUNGUZA UAGIZWAJI BIDHAA ZA KILIMO NJE YA NCHI

KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kinachofanyika leo Januari 29,2021 jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya,akisisitiza jambo kwa washiriki wa kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kinachofanyika leo Januari 29,2021 jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo na Maji Charles Mwijage,akizungumza kwenye kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kinachofanyika leo Januari 29,2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa ugani Tanzani (TSAEE) Prof.Catherine Msuya akielezea uimarishwaji wa huduma za Ugani wakati wa kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kinachofanyika leo Januari 29,2021 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wizara ya Kilimo Bw.Gungu Mubavu akielezea malengo na vipaumbele vya ASDP II kwenye kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kinachofanyika leo Januari 29,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Uratibu wa kisekta kutoka TAMISEMI,Enock Nyenda,akizungumzia uzoefu wa usimamizi wa huduma za ugani katika sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kinachofanyika leo Januari 29,2021 jijini Dodoma.  

Baaadhi ya washiriki wa Mkutano kutoka sehemu mbalimbali wakifatilia hotuba ya Katibu  Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kinachofanyika leo Januari 29,2021 jijini Dodoma.

Sehemu ya Wabunge wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo na Maji wakifatilia kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kinachofanyika leo Januari 29,2021 jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo bwana Gerald Kusaya, amewataka wataalamu wa kilimo na

maafisa ugani na wadau hapa nchini kuhakikisha wanatengezeza mfumo mzuri utakaoweza  kuliondoa Taifa katika utegemezi wa kuagiza  bidhaa za kilimo nje ya nchi ili kuipunguzia serikali mzigo wa kutumia kiasi kikubwa fedha kila mwaka kuagiza bidhaa hizo. 

Katibu Mkuu Kusaya ameyabainisha hayo Jijini Dodoma leo wakati  akifungua kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kinachofanyika Dodoma amesema kuwa taifa linatumia  kiasi kikubwa cha fedha katika kuagiza bidhaa mbalimbali nje ya nchi ambazo zingeweza kuzalishwa hapa nchini

“Hivi sasa taifa limekuwa na utegemezi mkubwa wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na mazao ya kilimo kama vile ngano, mafuta ya kula pamoja na sukari” amesema Kusaya.

Aidha Kusaya  amesema kila mwaka taifa  limekuwa likitumia kiasi cha Sh. bilioni 470, kila mwaka kwa ajili ya kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi lakini Kilimo kingesimamiwa vizuri na kwa hamasa kubwa fedha isingetumika nyingi kiasi hicho.

Ameongeza kuwa “Pia serikali imekua ikitumia kiasi cha Sh. bilioni 1.03 kila mwaka kwa ajili ya kuagiza unga wa ngano nje ya nchi kiasi ambacho ni mzigo mkubwa kwa taifa” amesema.

Kusaya amesema kutokana na hali hiyo maafisa kilimo kote nchini wanatakiwa kuwasaidia wakulima kulima kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi wa taifa na wao binafsi na kuondoa utegemezi kwa kiasi hicho.

Kusaya ameongeza kuwa “Tukiweka tija kwenye kilimo tutapiga hatua katika kuondokana na changamoto ya utegemezi kwa bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo, kama hivi sasa taifa linakabiliwa na upungufu wa tani 60,000 za sukari lakini kama tungekuwa tumejipanga vizuri kupitia wataalamu wetu hali hii isingekuwepo,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo na Maji Charles Mwijage, amesema kama serikali haitafanya uwekezaji mkubwa katika setka ya kilimo uchumi wa viwanda itakuwa ni ndoto kuufikia.

Mhe. Mwijage, amebainisha kuwa kutokana na sekta za kilimo na mifugo kuwajumuisha watu wengi kuna kila sababu ya uwekezaji wake kuwa kama ilivyo kwenye miradi mikubwa ya kimkakati hapa nchini kama taifa lingefikia malengo.

Mhe. Mwijage ameongeza kuwa “Sekta hizi za uzalishaji zikisimamiwa kwa kiwango cha juu katika taifa letu tutapiga hatua kubwa kiuchumi pamoja na kuondokana na umaskini” amesema Mwijage.

 

No comments :

Post a Comment