Tuesday, January 19, 2021

KOKA AIDHINISHA MILIONI 24.8 KATIKA MIRADI YA MAENDELEO


………………………………………………………….
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MBUNGE wa jimbo la Kibaha Mjini,Silvestry Koka ,ameidhinisha kiasi cha sh.milioni 24.8 , kupitia Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ,kwa ajili ya Kuchochea Miradi mbalimbali ya wananchi.

Alisema kati ya fedha hiyo ,milioni 9.800 zitaelekezwa kwenye kutengeneza madawati ya Shule za Msingi na Sekondari jimboni humo.

“Sh.milioni 1,000,000/- Kuchangia nguvu za wananchi kuweka kalvati mtaa wa Tangini, milioni 2,000,000/- Kuchochea nguvu za wananchi kwenye Ujenzi wa shule mpya ya Msingi Mkombozi kata ya Pangani”

1,000,000/- Kuendeleza Ujenzi wa Madarasa ya shule mpya ya Miembesaba A.”anasema Koka.

Alielezea,milioni 2,000,000 zitakuwa kwa ajili ya kuchangia Ujenzi wa Vyoo shule mpya ya Sekondari ya Viziwaziwa.

Pamoja na hayo,kiasi cha sh.1,000,000/- Kuchangia nguvu za wananchi kuweka Mbao kwenye daraja la muda la Lumumba- Kibwegere.

Mbunge huyo alibainisha kwamba,milioni 8 zitatumika katika Ujenzi wa darasa moja shule ya Sekondari Visiga.

Koka alifafanua,amekuwa akisaidia na kushirikiana na jamii kupitia fedha za mfuko wa jimbo na fedha zake na kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Alisema, fedha za mfuko wa jimbo hazitoshelezi lakini wamekuwa wakizigawa kutatua miradi mbalimbali ya maendeleo hatua kwa hatua.

 

No comments :

Post a Comment