Wednesday, January 20, 2021

DONALD TRUMP, MKEWE WAONDOKA IKULU



 DONALD Trump, Rais wa 45 wa Marekani  ameondoka Ikulu akiambatana na mkewe Melania Trump na hawatahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais mteule wa taifa hilo Joe Biden leo.

 Trump aliwasili katika uwanja wa Joint Base Andrews kabla ya kuelekea Palm Beach, Florida, ambapo  ametoa shukrani kwa wafuasi wake akiahidi kuwapigania, kuangalia na kusikiliza kinachoendelea katika Taifa hilo kuahidi  kurudi kwa namna nyingine. 

Makamu wa Rais Mike Pence hajaambatana na Trump na atahudhuria uapisho wa Joe Biden leo.

 

No comments :

Post a Comment