Mkuu
wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
akipanda mti wa kumbukumbu alipotembelea ndaki ya Dar es Salaam kituo
cha Tegeta.
Mkuu
wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
akimwagilia mti mara baada ya kupanda katika viwanja vya Kituo cha
Tegeta cha Ndaki ya Dar es Salaam ya Chuo Kikuu Mzumbe.Mkuu
wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
akizungumza na wafanyakazi wa Ndaki ya Dar es Salaam-Upanga ya Chuo
Kikuu Mzumbe.
Mwenyekiti
wa Baraza la Chuo Chuo Kikuu Mzumbe, Mhandisi Profesa Metthew Luhanga
akizungumza na wafanyakazi wa chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam
wakati wa Ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Lughano Kusiluka akizngumza na wafanyakazi wa Kampasi ya Dar es Salaam wakati wa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipotembelea katika ndaki hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakari Kunenge akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipotembelea kamapasi ya Dar es Salaam.
Rasi
wa Ndaki ya Dar es Salaam, chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest Ngowi
akizungumza na wafanyakazi wa Ndaki ya Dar es Salaam wakati wa ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Chuo Kikuu Mzumbe, Rose Joseph akizungumza wakati wa wakati wa ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu
wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
alipotembelea Kamapasi ya Dar es Salaam Kituo cha Tegeta.
Picha za Pamoja.
Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest Ngowi akisalimiana na Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo wakati wa ziara ya Mkuu wa Chuo
Kikuu Mzumbe alipotemelea Ndaki ya Dar es Salaa kituo cha Tegeta.
MKUU
wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Ali Mohamed Shein amewaasa wafanyakazi wa
Chuo hicho kuwa wazalendo katika kukipaisha chuo ili waombaji wa elimu
ya juu waweze kukikimbilia katika chuo hicho kikongwe ili kuendeleza
taaluma zao.
Hayo
ameyasema wakati wa kutambulishwa rasmi katika Ndaki ya Dar es Salaam
ya Chuo Kikuu Mzumbe wakati alipofika kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa
kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Januari 5, 2021. Amesema kuwa
wafanyakazi kama hawatashirikiana hawatatimiza malengo ya Chuo.
"Na
kazi yenyewe haiwezi kufanywa na mtu mmoja, kazi hufanywa na sisi sote
kila mmoja kwa nafasi yake, kila mmoja kwa wadhifa wake, kila mmoja
kufanya kile alichopangiwa kwahiyo ni kazi yetu sote na sisi tuchukue
mpango wa kupigania elimu na ubora wake pamoja na kukipaisha chuo chetu
ili kiwe bora zaidi na watu wakikimbilie zaidi." Amesema Dkt. Shein.
Hata
hivyo amesisitiza uzalendo kwa wafanyakazi wote na kuwa na ushirikiano
kwani mipango mingi iliyopangwa lazima itimie kwa kushirikiano ili
kukisaidia chuo kikuu hicho kiweze kundelea.
"Nasisitiza
umuhimu wa wafanyakazi kushirikiana kwa pamoja, katika lengo kuu la
nchi yetu ni kuinua sasa Chuo Kikuu Mzumbe kwani Mzumbe tunakila kitu,
kuna Baraza la chuo, mwenyekiti, katibu,Mzumbe tunaseneti, kunamajengo
mapya kwahiyo lengo letu la kuleta maendeleo katika elimu. Litatimia
hili tukishirikiana pamoja. Amesema Dkt.Shein."
Dkt.
Shein amesema kuwa katika kuhakikisha elimu hapa nchini inakuwa bora
zaidi lazima kuhakikisha maendeleo yanakuwepo katika kuboresha elimu
zaidi ili kuwa na viongozi wenye maono yenye maendeleo kwa taifa letu.
Lakini Dkt. Shein amewaasa kuanzisha programu ambazo zinahitajika zaidi ili kutatua changamoto katika jamii.
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka
alimshukuru kwa kutembelea Chuo Kikuu Mzumbe na kuahidi kushirikiana na
mkuu na Dkt. Shein.
Hata hivyo amemuahidi kupokea ushauri atakaoutoa kwani anauzoefu mkubwa katika kuongoza vyuo vikuu hapa nchini.
Katika
Ziara hiyo Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Shein amepata taarifa fupi
ya maendeleo ya ndaki hiyo, alizungumza na wafanyakazi wa ndaki ya Dar
es Salaa-Upanga na kisha kuelekea Kituo cha Tegeta ambapo alipata nafasi
ya Kuzungumza na wanafuzi wanaosoma shahada ya kwanza pamoja na kupanda mti wa kumbukumbu.
Miongoni
mwa Viongozi alioambatana nao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Abubakari Kunenge na Mkuu wa wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo.
No comments :
Post a Comment