Monday, January 25, 2021

DKT.MPANGO ATOA ONYO KWA WATUMISHI WA WIZARA HIYO WANAOKIUKA TARATIBU ZA KAZI YAO.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip  Mpango akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo wakati  akifungua Mkutano wa Baraza la wafanyakazi hao ulilofanyika leo Januari 25,2021  jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Januari 25,2021  jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu(utawala) wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga akitoa neno la shukrani kwa  mgeni rasmi mara baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Januari 25,2021  jijini Dodoma.
Baadhi yawashiriki   wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philipo Mpango wakati akifungua Mkutano huo uliofanyika leo Januari 25,2021  jijini Dodoma.
…………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt  Philip Mpango amelitaka baraza la wafanyakazi Wizara hiyo

  kufanyakazi kwa kufuata misingi yao na hatasita kumchukulia hatua mtumishi atakayebainika kukiuka misingi na kutoa siri na taarifa nyeti za serikali.

 Dkt. Mpango ameyabainisha hayo leo Januari 25,2021 Jijini Dodoma  wakati alipokuwa akifungua   mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo amesema mtumishi yeyote atakayekiuka taratibu na miongozo hatavumilika.

“Natanguliza onyo kali kwa mtumishi yeyote atakayebainika kukiuka taratibu ,miongozo na miiko ya kazi yake ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango utajutia ukaidi wake” amesema Dkt Mpango.

Aidha amesema wafanyakazi hao kuwa wana majukumu makubwa katika mstakabali wa Taifa hasa wakati huu wa kutekeleza bajeti ya serikali katika majukumu yake.

“Hii ina maana tunaowajibu wa kuongeza tija na ufanisi katika kutekeleza  majukumu yetu na naamini kuwa mtatumia mkutano huu kutathimini utendaji kazi,” amesema.

Pia ametaka viongozi hao kuwa na utaratibu wa kuwasikiliza watumishi ili kupunguza au kuondoa malalamiko  na manung’uniko ya wafanyakazi pindi wanapokuwa kazini ili wafanyekazi kwa utulivu kufikia malengo.

Ameongeza kuwa “Lazima tutambue  na kukubali kuwa ufanisi sehemu ya kazi hutegemea uhusiano uliopo baini ya viongozi na wafanyakazi ,hivyo basi nawaasa viongozi wenzangu tufanye kila tuwezalo kujenga uhusiano mzuri” amesema.

Awali  Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara fedha na mipango, bwana Doto James amesema mkutano huo utakuwa pamoja na mambo mengine watachagua viongozi wapya pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali kuboresha utendaji kazi.

 

No comments :

Post a Comment