Meneja Mwandamizi Ukusanyaji wa Amana Benki ya CRDB, Abel Lasway (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi Kampeni ya Benki hiyo iliyotambulika kama "Tumekusoti Ada" iliyoendeshwa katika kipindi cha mwezi wa Disemba kwa wateja waliofungua akaunti ya watoto (Junior Jumbo) na kuweka akiba ambapo jumla ya wateja 20 wameibuka washindi. Wengine pichani ni Meneja Mauzo wa Benki ya CRDB, Elikira Nkya (kulia) pamoja na Meneja Mahusiano wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Bupe Makibi .
Benki
ya CRDB imetangaza washindi wa promosheni ya “Tumekusoti Ada”
iliyozinduliwa na Benki hiyo mapema mwezi Disemba ikilenga katika
kuhamasisha wazazi/ walezi kujenga utamadani wa kuwawekea akiba watoto
wao kupitia Akaunti ya Junior Jumbo (JJ).
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Meneja Mwandamizi Ukusanyaji wa
Amana Benki ya CRDB, Abel Lasway amesema jumla ya shilingi milioni 30
zimetolewa kama zawadi ya ada kwa washindi 20 ambapo kila mmoja
amepatiwa shilingi milioni 1.5.
Akielezea
namna ambavyo washindi hao wamepatikana Lasway alisema zawadi
zimetolewa kwa wazazi ambao wamekuwa wakiweka akiba mara kwa mara katika
akaunti ya Junior Jumbo ya watoto wao.
“..
tumefanya hivi ili kujenga utamaduni wa kwa wazazi/ walezi kuwawekea
watoto wao akiba. Hii inasaidia wazazi kumudu gharama zote zinazohusu
watoto ikiwamo ada, matibabu na gharama nyinginezo bila shida yoyote,”
alisema Lasway.
Lasway
alisema wazazi wengi wamekuwa wakipata changamoto katika kulipa ada za
watoto kutokana na wengi kutokuwa na utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili
ya watoto. Hali hiyo imepelekea watoto wengi kuchelewa kurudi shule
kuendelea na masomo au kujiunga na shule kwa wanafunzi wapi kutokana na
kukosa kwa mahitaji ya msingi ikiwamo ada.
“Tuna
akaunti maalum kwa ajili ya kusaidia wateja kuweka akiba kwa ajili ya
watoto, na hii si nyengine ni akaunti ya Junior Jumbo, ni akaunti ambayo
inafunguliwa kwa vigezo nafuu sana, haina makato yoyote na hutoa faida
ya riba kwa mteja,” anasema Adili huku akisisitiza kuwa Benki ya CRDB
imejipanga kutoa elimu kwa wazazi ili kuwasaidia kuishi ndoto za watoto
wao kwa kumuwezesha kupata elimu bora.
Lasway
alitoa rai kwa wazazi ambao bado hawajawafungulia akaunti watoto wao
kutembelea matawi ya Benki ya CRDB yaliyopo nchi nzima kwa ajili ya
kufungua akaunti na kuanza kuwawekekea akiba. Aliwataka wazazi pia
kuwafundisha watoto kujiwekea akiba wenyewe katika akaunti zao jambo
litakalosaidia kuwajenga katika kuweka akiba na matumizi sahihi ya
fedha.
Lasway
alisema Benki hiyo imerahisisha kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma zake
kwa kuwekeza katika mifumo ya kidijitali inayowawezesha wateja kupata
huduma popote pale walipo na kwa urahisi.
“Kupitia
njia hizi za kidijitali kama SimBanking, SimAccount, Internet Banking
mzazi anaweza kuweka fedha moja kwa moja katika akaunti ya Junior Jumbo
ya mtoto bila ya kutembelea tawini,” alisema Lasway huku akibainisha
wateja pia wanaweza kuweka fedha katika akaunti kwa kuhamisha moja kwa
moja kutoka katika mitandandao ya simu.
No comments :
Post a Comment