*************************************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo amepokea mchango wa Madawati 400
kutoka Bank ya NMB kwaajili ya kusaidia tatizo la uhaba wa Madawati
Jijini humo ambapo ametoa wito kwa Wadau kuendelea kuchangia sekta ya
elimu.
RC Kunenge amesema
mpaka kufikia siku ya leo Wamefanikiwa kukamilisha Ujenzi wa Vyumba vya
Madarasa 97 kati ya 339 kwaajili ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na
kidato Cha Kwanza na kukosa nafasi ambapo amebainisha Hadi kufikia
February 28 madarasa yote yatakuwa yamekamilika ikiwa ni utekelezaji wa
agizo la waziri Mkuu.
Aidha RC Kunenge
ameishukuru Bank ya NMB kwa kutoa mchango huo ambao kwa kiasi kikubwa
utaenda kupunguza tatizo la uhaba wa Madawati ambapo amesema mbali na
ujenzi wa madarasa pia wanaendelea na ujenzi wa Madawati takribani
40,000 ambayo yapo Katika hatua nzuri ya kukamilika.
Akikabidhi Madawati
hayo, Kaimu Afisa Mkuu wa fedha wa Bank ya NMB Bwana Benedicto Baragomwa
amesema Madawati hayo yatagawanywa Katika Shule mbalimbali ambapo Shule
ya Msingi King’ongo itapatiwa Madawati 150 na Madawati yaliyosalia
yatakabidhiwa kwa shule nyingine.
Hata hivyo Bwana
Baragomwa amesema Bank hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mkoa
huo Katika masuala mbalimbali ya kijamii.
No comments :
Post a Comment