Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimpa maelezo Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar juu ya ubora wa bidhaa za kiwanda cha kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimpa maelezo Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar juu ya ubora wa bidhaa za kiwanda
cha kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini
huku akiwa ameshika moja ya bidhaa za IVORI Iringa.
…………………………………………………………………………………….
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar amekipongeza
kiwanda cha kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa
mjini,ambacho kimekuwa kikizalisha bidhaa zenye ubora kwa matumizi ya
binadam yeyeto yule wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Akizungumza wakati
alipotembelea banda la bidhaa za IVORI Iringa wakati wa maonyesho ya
kibiashara ya mkoani Iringa yaliyofanyika katika chuo cha Mkwawa balozi David Concar alisema kuwa amepongeza uzalishaji wa pipi,chocolate, tomato source na bidhaa nyingi zilivyo bora.
Balozi Concar alisema
kuwa ameonja bdhiaa za IVORI Iringa na kupata radhaa nzuri tofauti na
bidhaa nyingine zinzotengenezwa kwenye viwanda vingine kama pipi na
chocolate.
Alisema kuwa
amevutiwa na bidhaa za kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd
ya Iringa mjini, na kuahidi kuitangaza kokote kule atakapokuwa ametembea
kutoka na kuvutiwa na jinsi ya uzalishwaji wake ulivyokuwa na bora wa
kimataifa.
Balozi Concar
aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho cha uzalishaji bidhaa za IVORI
Iringa kuhakikisha wanatanua na kujitangaza zaidi kitaifa na kimataifa
kwa sababu ametembea kwenye super market nyingi hajaona maji ya kampuni
hiyo ambayo yeye anaamni kuwa ndio kampuni yenye bidhaa bora hapa
nchini.
Akiwa ameambatana na
balozi wa uingereza nchini Tanzania, mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela alisema kuwa amekuwa balozi wa kujitegemea kuzitangaza bidhaa
za IVORI Iringa kila kona ya Tanzania kutokana na ubora wake.
Alisema kuwa
anamuomba balozi huyo awe balozi wa kutangaza bidhaa zinazotengezwa
na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa
mjini, kutokana na ubora wake.
Kasesela aliwataka viongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanatanua wigo wa masoko ya bidhaa.
Alisisitiza wananchi
wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa wataendelea kutumia bidhaa za
IVORI Iringa kwa kuwa ni bora na salama kwa matumizi kwa binadamu
yeyote yule.
Kwa upande wao baadhi
ya wanachi mkoani Iringa waliohudhulia katika maonyesho hayo
yaliyofanyikia katika chuo cha Mkwawa walizipongeza bidhaa za IVORI
Iringa kwa ubora wake kwa kuwa wamekuwa wakizumia Mara kwa Mara.
Walisisistiza kuwa
wataendelea kuzitumia bidhaa za IVORI Iringa kila Mara wanapokuwa na
uhitaji wa bidhaa za aina hiyo lakini wanatakiwa kuhakikisha wanaulinda
na kuuboresha ubora wake ambao upo hadi hivi sasa.
Kwa upande wake afisa masoko wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini Moyo
Machea alisema kuwa mali ghafi zote wanazotumia kuzalishia bidhaa hizo zinapatikana hapa nchini na hasa mkoani Iringa.
Alisema
kuwa changamoto wanayokabiliana ni kupanda mara kwa mara kwa Mali ghafi
zinatotumiwa viwandani kama vile sukari na unga wa ngano na changamoto
hiyo sio kwa viwanda tu bali hata kwa wananchi wa kawaida wanakubwa
changamoto ya kupanda kwa bei.
Machea
alisema kuwa maonyesho hayo ya kibiashara yanafaida kwa wananchi na
wafanyabishara kutambua fursa mbalimbali ambazo zitasaidia kuleta
maendeleo.
“Haya
maonyesho yanasaidia kutambua fursa mbalimbali katika maisha tunayoishi
kutokana na kuona kwa bidhaa ambazo zilizopo kwenye maonyesho kwa
wafanyabishara inatoa fursa ya kujitangaza na kutangaza bidhaa
zao”alisema Machea
Alisema kuwa kwasasa hakuna tatizo kubwa la soko kwa bidhaa za kampuni
ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini kutokana
kampuni hiyo kutengeneza bidhaa bora zinazohotajika katika soko la sasa.
Machea aliwapongeza viongozi wa serikali na wadau mbalimbali waliofanikisha maonyesho hayo kufanikiwa kwa kiasi kikubwa
Alimazia kwa kuwaomba
wananchi wa nchini Tanzania na nje ya nchi kuendelea kutumia bidhaa
bora zinazozalishwa na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd
ya Iringa mjini.
No comments :
Post a Comment