Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Bw. Edward Mbanga akiongea na wataalam wa tiba asili/mbadala kutoka
taasisi za serikali na vyuo vikuu mbalimbali vinavyojishughulisha na
tafiti za dawa za tiba asili nchini
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Eliud Eliakimu akizungumza wakati wa kikao hicho
Kaimu Katibu Mkuu Edward Mbanga (katikati) na Kaimu Mganga Mkuu wa
Serikali Dkt. Eliud Eliakimu(kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Dkt.
Grace Maghembe wakifuatilia uwasilishaji wa mada kwenye kikao cha
kujadili muelekeo wa tiba asili nchini. Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa kikao kazi cha kujadili muelekeo wa tiba asili na tiba mbadala nchini
Mkemia Mkuu wa Serikali kutoka
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko na
Msajili wa Baraza la Tiba Asili/Mbadala Dkt. Ruth Suza wakifuatilia
ufunguzi wa kikao kazi hicho Wataalam wa tiba asili/mbadala wakifuatilia hotuba ya ufunguzi toka kwa Kaimu Katibu Mkuu-Idara kuu Afya
Washiriki wa kikao kazi cha siku
mbili cha kujadili muelekeo wa tiba asili nchini kinachofanyika kwenye
ukumbi wa ofisi za wizara zilizopo Area D jijini Dodoma.
(Picha zote na Rayson Mwaisemba-WAMJW)
***************************************
Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma
Wataalam wa tiba asili na tiba
mbadala nchi wametakiwa kufanya utafiti ambao utakuwa na ushahidi wa
usalama wa dawa pamoja na ufanisi wa wa dawa hizo kwa watumiaji.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu
Katibu Mkuu wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na
watoto-Idara kuu Afya Bw. Edward Mbanga wakati wa kikao cha pamoja cha
wizara na wataalam hao kutoka taasisi za Serikali na Vyuo Vikuu
mbalimbali nchini kilichofanyika kwenye ukumbi wa wizara jijini Dodoma.
Mbanga amesema kuwa ushahidi
huonekana kwenye utafiti hivyo warudi nyuma na kujiuliza wamekosea wapi
na nini kifanyike ili kuwa na uelewa wa pamoja kwani kizazi kijacho
kinahitaji kuelezwa na kuelewa tiba asili.
“Lazima tuulizane tunataka
kufikia wapi na kuweka mikakati ya kuyafikia,nashauri tutambue nini
kifanyike,tuna changamoto zipi na tunafikaje huko kwa kushirikiana kwa
pamoja ili tutambue kwanini hatufiki hivyo lazima tujikite kwenye
utafiti wenye ushahidi”.Alisisitiza.
Aliongeza kuwa katika kikao
hicho wataalam hao wanatakiwa kutafuta majibu ambayo tiba asili
itaendelea hata baada ya kipindi hiki,na wawe na matamanio kama nchi
nyingine ili tiba asili itolewe kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
nchini.
“Tumekuwa tukifanya utafiti wa
masuala ya tiba asili na tiba mbadala kuanzia miaka ya sitini, sasa
tujiulize tangu tutafiti hadi sasa matokeo yanafanana?,bado kuna
changamoto ya watu kushindwa kuthamini vya kwao hasa katika matumizi ya
tiba asili kwa kuamini vinavyotoka nje ya nchi vina ubora zaidi kuliko
vya kwao.
Hata hivyo Kaimu katibu mkuu
huyo aliwataka katika kikao hicho watoke na mkakati wa kuanzisha vituo
vya uendelezaji vya tiba asili kwenye halmashauri zote kwa kuwapatia
ujuzi na motisha wataalam wa tiba asili pamoja na kufanyia tafiti dawa
zao na mwisho wa utafiti kuwe na haki miliki.
Kwa upande wake Kaimu Mganga
Mguu wa Serikali Dkt. Eliud Eliakimu amesema kuwa kama nchi wameamua
kuendeleza tiba asili kwa umoja ili kuwe na spidi ambayo italeta
mafanikio yenye tija nchini.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Tiba
kutoka Wizara ya afya Dkt. Grace Maghembe amesema tiba asili zipo na
zinatumika kutibu magonjwa mbalimbali na malighafi ya kutengeneza dawa
hizo zipo hapa nchini hivyo uwezo wa kutengeneza katika viwango kama
nchini nyingine inawezekana endapo kutawekwa msukumo na hivyo kusaidia
kuinua uchumi wa nchi na wa wakulima wa hapa nchini.
No comments :
Post a Comment