Saturday, December 12, 2020

UTALII- MASHIRIKA YA NDEGE YA KIMATAIFA YAONGEZA SAFARI TANZANIA

***************************************

Shirika la Ndege la Uholanzi (KLM) limeanzisha safari zake nchini Tanzania ambapo litafanya

safari zake mara mbili kwa wiki Zanzibar. Mara nne katika kiwanja cha Kilimanjaro na kisha kuelekea Dar es salaam na kurudi Amsterdam. Mashirika mengi ya Ndege yanavutiwa na uwepo wa abiria wengi wanaotembelea Tanzania hususani watalii.

Aidha, pamoja na changamoto zilizojitokeza Tanzania imeendelea kufanya vizuri kimataifa katika utalii, Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda tuzo ya hifadhi bora barani Afrika kwa mwaka 2020. Tuzo hizi zinazotolewa na taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani na hii ni mara ya pili kwa hifadhi ya Serengeti kushinda katika kundi la hifadhi zinazoongoza kwa ubora zaidi bara la Afrika baada ya kushinda pia mwaka jana 2019.

Serikali ya Tanzania imeendelea kuimarisha sekta ya utalii nchini Tanzania kwa kusimamia ipasavyo mikakati ya kukuza vivutio ili kuhakikisha Watanzania wengi hususani vijana wananufaika kwa kupata ajira na kuongeza kipato. Licha ya faida za kiuchumi zitokanazo na utalii , Tanzania ni kati ya vinara katika kukabiliana na uwindaji haramu (poaching) kwaajili ya mustakabali endelevu wa uhifadhi wa mifumo ya ekolojia.

 

No comments :

Post a Comment