Thursday, December 10, 2020

SERIKALI YAWATAKA WANAHABARI KUSHIRIKI KUIELIMISHA JAMII KUSIMAMIA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wanahabari jana kuhusu Kongamano la Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu litakalofanyika leo Disemba 10, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akijibu maswali ya wanahabari kuhusu Kongamano la Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu litakalofanyika leo Disemba 10, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF jijini Dodoma.

Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akizungumza nao jana kuhusiana na Kongamano la Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu litakalofanyika leo Disemba 10, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF jijini Dodoma.

*********************************

Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 10 Disemba, 2020.

Wanahabari kutoka katika Vyombo mbalimbali vya Habari wametakiwa kuisaidia Serikali

kuielimisha jamii ili kila mwananchi atambue kuwa, kwa nafasi aliyonayo anao wajibu wa kuhakikisha jamii inakuwa na maadili mema, inaheshimu haki za binadamu na kushiriki vita dhidi ya rushwa.

Wito huo umetolewa jana jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb), wakati akizungumza na Wanahabari kuhusu Kongamano la Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu litakalofanyika Disemba 10, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF Dodoma.

Mhe. Mkuchika amewataka wanahabari kuueleza umma mafanikio ya Serikali katika kuimarisha maadili, mapambano dhidi ya rushwa na uzingatiaji wa haki za binadamu.

Mhe. Mkuchika amesisitiza kuwa, ni muhimu wananchi waelewe jitihada ziizofanywa na Serikali kuimarisha maadili kwa jamii, kupambana na rushwa na kusimamia haki za binadamu ili waunge mkono jitihada hizo.

Aidha, Mhe. Mkuchika amesema, kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kwa mwaka huu 2020 ni; Uzingatiaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi na Watumishi kwa Ustawi wa Utawala Bora na Haki za Binadamu.

Maadhimisho ya mwaka huu, yataadhimishwa kwa Kongamano litakalofanyika leo Disemba 10, 2020 na kuhudhuriwa na Wadau wa Sekta ya Sekta ya Umma, Sekta Binafsi, Taasisi zisizo za Kiserikali na Wabia wa Maendeleo.

 

No comments :

Post a Comment