Serikali
imeahidi kugharamia mazishi ya watu wawili waliofariki baada ya
kudondokewa na jen-go maarufu la kitalii, Beit Al Ajaib (Jumba la
Maajabu) lililopo eneo la Mji Mkongwe mjini Unguja visiwani Zanzibar.
Waliofariki
ni Pande Haji Makame (39) na Burhani Ameir Makuno (34) walibainika kati
ya saa sita na saa nane usiku kwenye jitihada za kuwatafuta
waliofunikwa na kifusi cha jengo hilo.
Wakati
wawili hao wakitolewa katika kifusi, wengine wanne walikuwa wakitibiwa
majereha waliyoyapata katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Jumba hilo maarufu lililodumu kwa zaidi ya miaka 130 lilidondoka juzi mchana na kuwafunika mafundi waliokuwa wakilikarabati.
Jana Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla akifuatana na mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya aliwatembelea majeruhi waliolazwa na kwenda eneo la tukio
Katika
hatua nyingine, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amevitaka vyombo
vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini chanzo cha
kuporomoka kwa sehemu ya jengo la makumbusho la Taifa la Beit al Ajab.
No comments :
Post a Comment