Mkurugenzi
Mkuu wa SAGCOT Godffrey Kirenga akizungumza mbele ya Waandishi wa
Habari leo jijini Dar,akiipongeza TAHA kwa kuandaa kongamano hilo
muhimu ambalo
litajadili mustakabali kuhusu kilimo cha mbogamboga na matunda,kushoto
ni Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka TIC John Mnali
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KITUO
cha Uwekezaji Tanzania(TIC) pamoja na Taasisi ya Kuendeleza Kilimo
Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) wamezungumzia umuhimu wa
kilimo cha mbogamboga na
TIC na SAGCOT wamesema hayo leo wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam uliokuwa unazungumzia kongamano kubwa ambalo limeandaliwa na Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Asasi ya Mazao ya Bustani(TAHA) litakalofanyika Desemba 5,2020 na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa SAGCOT Godffrey Kirenga amesema wanapongeza TAHA na wadau
wengine kwa kuandaa kongamano hilo muhimu ambalo litajadili mustakabali
kuhusu kilimo cha mbogamboga na matunda."Ni muhimu kueleza kuna safari
tumepitia katika miongo miwili iliyopita wakati sekta hii ikiwa
haijulikani.
"Ilikuwa pembeni kidogo lakini nafurahi katika
juhudi ambazo zimefanywa na TAHA na wadau wengine hii sekta imeeanza
kuonekana moja ya sekta muhimu na kongozi katika sekta ya kilimo.Jambo
muhimu katika huu mkutano.
"Kwanza kabisa kutekeleza maagizo ya Serikali, nakumbuka wakati wa ufunguzi wa Bunge la 12 , ilitolewa hotuba na Rais na jambo ambalo lilinifurahisha mimi na wadau wengine wa kilimo ni mikakati iliyopo kwenye kilimo,"amesema.
Ameongeza
maeneo yanayokuwa kwa kasi katika kilimo ni pamoja na sekta ya
mbogamboga na matunda ingawa wengi hawafahamu kwani inakuwa kwa asilia
15 kwa mwaka ukuaji, hivyo ukiweka mchango wake katika kilimo ni mkubwa.
"Sekta
hii ya mbogamboga na matunda ni muhimu , na tunapata eneo jingine la
kuufahamisha umma wa watanzania kwamba Tanzania iko katika ramani katika
kuzalisha mboga na matunda kwa ajili ya kuuza soko la ndani na nchi
jirani. "Sisi tunafanya kazi sana ukanda wa Kusini lakini haina maana
kwamba tumesahau maeneo mengine, hivyo kuna umuhimu wa kuchagua ni wapi
tutawekeza juhudi hizi,"amesema.
Aidha
amesema kilimo cha mbogamboga na matunda kinahitaji ufahamu wa namna ya
kuzalisha hayo mazao, kinahitaji miudombinu na kujipanga,hivyo lazima
uwe na mbegu bora, pembejeo , kuhifadhi mazao pamoja na umuhimu wa kuwa
na sera zinazotabarika ambazo zinatoa fursa za mtu kuwekeza.
"Ukiwa
na sera zinazotabirika itasaidia wananchi wa Tanzania kuwekeza katika
kilimo hiki, na katika eneo ambalo linatoa ajira kwa haraka ni eneo hili
la kilimo cha mbogamboga na matunda.Kupitia mkutano huu naamini
tutatoka na majibu ya nini cha kufanya katika kuendeleza kilimo hiki.
Hata
hivyo ni muhimu kwa waandishi wa habari kuendelea kutumia vyombo vyenu
kuendelea kutupasha habari kuhusu fursa ambazo zinapatikana katika
kilimo hiki,mkutano huu unakuja kufunguliwa na Wziri Mkuu kwetu hii ni
heshima kubwa,"amesema Kirenga.
kilimo cha nchi zilizoendelea
kimejikita kwenye kilimo cha mbogamboga, ukiondoa mazao yale ya zaman,
serikali inatoa kipaumbele hivyo ni muhimu kuendelea kuhamasisha
uwekezaji kwenye eneo hilo.
Kwa upande Mkurugenzi wa Uhamasishaji
Uwekezaji kutoka TIC John Mnali amesema wao na TAHA ni wadau wakubwa na
wanafanya kazi kwa ukaribu, hasa maeneo yale ambayo yamelengwa katika
kuhamasisha na kuvutia uwekezaji nchini ikiwemo sekta ya matunda na
mbogamboga.
"Kwa hiyo kwa kiasi kikubwa tunafanya kazi kwa karibu sana, na kwa upande mwingine niseme tu TAHA wamekuwa wa msaada kwa kituo cha uwekezaji kwani kupitia shughuli zao wanazofanya wamekuwa mabalozi wetu wa kutangaza fursa za uwekezaji mbalimbali.
"Kupitia mkutano huu wale wawekezaji watakaonesha nia ya kuwekeza katika maeneo mbalimbali yanayosimamiwa na TAHA, kituo cha uwekezaji tutakuwa na jukumu la kuhakikisha wanapata vibali na leseni wanazohitaji kwa wakati, kama mavyofahamu kituo cha uwekezaji kimehamishiwa ofisi ya Rais."Na majukumu yetu yameongezeka zaidi, ufahamu wetu umeongezeka zaidi, tumejipanga kuhakikisha vile vikwazo kwa wawekezaji vilivyokuwepo hapo zamani vinatafutiwa suluhu.Hivyo wawekezaji wasiwe na wasiwasi kuanzisha miradi yao,TIC tumejipanga,"amesema.
No comments :
Post a Comment