Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemteua
Prof. Shukrani Manya kuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Madini na ataapishwa
leo mchana Ikulu Chamwino Dodoma.
Disemba
9,2020 Rais Magufuli alisema atafanya uteuzi wa Naibu Waziri mwingine
wa Madini baada ya aliyemteua, Francis Ndulane Kumba ambaye ni Mbunge wa
Kilwa Kaskazini kushindwa kuapa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Ndulane
ambaye ni mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM) mwenye elimu ya shahada ya
uzamili alikuwa mmoja wa waliotakiwa kuapa lakini alishindwa kusoma
kiapo mbele ya Rais Magufuli, akikosea mara kadhaa kila alipopewa nafasi
ya kurudia kusoma na ndipo katibu mkuu kiongozi, John Kijazi kumtaka
aende kuketi kwanza ili wenzake waendelee kuapa.
Ndulane alisitasita na kukosea, kurudia hadi alipokatizwa na kutakiwa kupumzika.
“Mimi
Francis Kumba Ndulane naapa kwamba,” akasimama kwa muda na kuendelea
“nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, kabla ya
kusimama tena kwa muda na kuanza upya kusoma kiapo kwa kasi kidogo.
“Mimi
Francis Kumba Ndulane naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na kwamba,” anasimama tena na kuinamia zaidi
karatasi yenye kiapo ili kusoma vizuri kabla ya kukkiinua juu na
kusogeza usoni na kuanza tena kusoma.
“Mimi
Francis Kumba Ndulane naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba
nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa mujibu wa sheria iliyowekwa. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.”
Alisoma
sehemu ya pili ya kiapo hicho kwa kutetereka tena na alipomaliza,
Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi alimtaka arudie tena kusoma kiapo.
Safari ya pili alisita zaidi hadi walipomkatisha na kumtaka arudi kupumzika.
Ndulane
ana elimu ya shahada ya uzamili katika uhasibu na fedha ambayo aliipata
Chuo Kikuu cha Mzumbe kati ya mwaka 2013 na 2015. Pia, ana stashahada
ya juu ya uhasibu kutoka Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM).
Ndulane
alisoma shule ya msingi Uwanjani (mwaka 1980 - 1986), baadaye akaenda
sekondari ya Tambaza (mwaka 1987 - 1990) na baada ya kuhitimu kidato cha
nne, alikwenda sekondari ya Pugu (mwaka 1991 - 1993) ambako alihitimu
kidato cha sita.
Ili
kupata shahada ya uzamili, Ndulane aliandika chapisho kuhusu changamoto
wanazopata makandarasi wadogo na wa kati na kuathiri utendaji wao.
No comments :
Post a Comment