Tuesday, December 15, 2020

PROF. KITILA AANZA KAZI NA TIC, ATAKA TAARIFA ZA UWEKEZAJI KILA BAADA YA MIEZI MITATU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akisikiliza jambo kutoka kwa Afisa wa Wizara ya Ardhi anayehudumia Wawekezaji katika Kituo cha Uwekezaji (TIC,) Kituo cha Huduma za Mahala za Pamoja (One Stop Centre).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akitoa maelekezo kwa Maafisa mbalimbali wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), katika Kituo cha Huduma za Mahala za Pamoja (One Stop Centre).

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji,) Prof. Kitila Mkumbo rasmi ameanza kazi kwa kutembelea Ofisi za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) zilizopo jijini Dar es Salaam, kuangalia utendeji kazi wa Kituo hicho na

kuhakikisha uhamasishaji Uwekezaji kutoka nje na ndani ya nchi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Prof. Kitila amesema amefika TIC kuwapa muelekeo wa Serikali ya awamu ya tano kuhusu Uwekezaji, pia kusisitiza kubadili mifumo ya utendaji, Mitazamo ili kuvutia Wawekezaji.

“Wawekezaji wa ndani wasisahaulike lazima wachukue nafasi yao, namna moja ya kusukuma Uchumi wetu ni kuvutia Uwekezaji wa ndani na nje.” ameeleza Prof. Kitila.

Prof. Kitila amesisitiza TIC kuhakikisha Wawekezaji kutoka nje ya nchi wanakamilishiwa taratibu za uwekezaji ndani ya siku 14, amesema jambo hilo linawezekana na tayari wamejipanga kukamilisha suala hilo, pia amewapa hamasa TIC kuhakikisha wanajulikana, kujitangaza kuhusu majukumu yao.

“Tunataka TIC ijitangaze Kimataifa, fursa za Uwekezaji Tanzania na namna ya kuwekeza kwa Wawekezaji wa Wakubwa duniani kupitia Majarida ya Kimataifa na Vyombo vya Kimataifa”, amesema Prof. Kitila.

Pia Prof. Kitila ameagiza kuripotiwa maendeleo ya Uwekezaji nchini Tanzania kila baada ya miezi mitatu, kutoa taarifa ya idadi ya Wawekezaji, maeneo ya Uwekezaji, kiasi cha mitaji ya Wawekezaji, ajira zinazozishwa, pia kuwa na mahusiano na Taasisi za Serikali. 

Katika ziara hiyo Kituoni hapo, Prof. Kitila ametembelea Kituo cha Huduma za Mahala za Pamoja (One Stop Centre) katika idara zake mbalimbali za Uhamiaji, Ardhi, Mamlaka ya Mapato (TRA), Baraza la Uhifadhi na Usimamizi  wa Mazingira (NEMC), Shirika la Viwango (TBS).

No comments :

Post a Comment