Waziri Mkuu Mstaafu mhe. Mizengo Pinda akihutubia washiriki wa Kongamano la kilele cha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu lililofanyika leo Desemba 10,2020 Jijini Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi. Waziri wa nchi , Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika (Mb) akieleza kuhusu maadhimisho ya kilele cha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu u leo Desemba 10,2020 Jijini Dodoma ambapo Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda alikuwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Utawala Bora kutoka UNDP hapa nchini Bw. Godfrey Mulisa akitoa tamko la Umoja huo kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini kuhusu rushwa na haki za binadamu leo Desemba 10,2020 Jijini Dodoma ambapo Waziri mkuu mstaafu mhe. Mizengo Pinda alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
Mweneyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji mstaafu Mathew Mahimu akieleza kwa washiriki faida za maadhimisho ya kilele cha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo Desemba 10,2020 Jijini Dodoma ambapo Waziri Mkuu Mstaafu mhe. Mizengo Pinda alikuwa mgeni rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali Charles Mbungo akitoa maelezo kuhusu kilele cha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo Desemba 10,2020 Jijini Dodoma ambapo Waziri mkuu mstaafu mhe. Mizengo Pinda alikuwa mgeni rasmi. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Ryoba (wakwanza kulia) akifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ya kilele cha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo Desemba 10,2020 Jijini Dodoma ambapo Waziri Mkuu mstaafu mhe. Mizengo Peter Pinda alikuwa mgeni rasmi.
***********************************
Na Jonas Kamaleki
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amewataka watumishi wa umma na wa sekta binafsi kujitathmini jinsi wanavyotoa huduma kwa wananchi ili kutoa huduma bora.
Waziri Mkuu Mstaafu Pinda ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua kongamano maalum la kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu.
Aliongeza kuwa mada zitakazotolewa kwenye kongamano hilo zitakuwa chachu katika kuwafanya washiriki kuzingatia uadilifu na utawala bora.
“Ahadi ya uadilifu ikitekelezwa, ninaamini kuwa na utoaji wa huduma kwa umma utaimarika na kuwa bora zaidi”, alisisitiza Mizengo Pinda.
Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejitahidi kuboresha utumishi wa umma kimaadili na kiutendaji na hivyo kuwafanya watanzania kuiamini na kuipenda Serikali yao.
“Kutungwa kwa sheria mbalimbali na kanuni za utumishi wa umma mathalani Sheria ya Utumishi wa Umma na kanuni zake,Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma, Mkakati wa Taifa dhidi ya Rushwa na miongozo mingine ya utumishi wa umma, yote hayo ni kuongoza watumishi wa Serikali katika kuwahudumia vizuri wananchi”, aliongeza Pinda.
Aidha, Pinda alisema ipo miongozo na maelekezo kwa sekta binafsi ambayo inalenga kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Mkakati wa Taifa dhidi ya Rushwa unazuia vitendo vya kutoa au kuomba hongo ili kutoa huduma kwa mteja jambo ambalo halikubaliki, alisisitiza Pinda.
Aliongeza kuwa utoaji wa taarifa za mapato uwe wa wazi bila kuwa na vitendo viovu katika suala hilo.
“Nitoe wito kwa viongozi wa umma na sekta binafsi kusimamia ahadi ya uadilifu katika maeneo yao ili kukomesha vitendo vya rushwa na utovu wa nidhamu”, alisisitiza Pinda na kuongeza kuwa juhudi za Rais John Pombe Magufuli dhidi ya rushwa na hatua nyingine za kukabiliana na uzembe zimeiletea sifa Tanzania hata nchi jirani wanasifia na kupongeza hatua hizo.
Kongamano hilo maalum linalofanyika jijini Dodoma lina Kauli Mbiu isemayo: “UZINGATIAJI WA AHADI YA UADILIFU KWA VIONGOZI NA WATUMISHI KWA USTAWI WA UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINADAMU NCHINI”.
No comments :
Post a Comment