Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakifurahia ‘NMB Friday’
Mkuu
wa Biashara ya Kadi wa Benki ya NMB – Philbert Casmir akionyesha baadhi
ya zawadi zinazotolewa kwa wateja katika kampeni ya Mastabata Siyo
Kikawaida zikiwemo; Friji, TV Simu na vinginevyo.
***********************************************
Benki
ya NMB imeendelea kuhakikisha wateja wao wanafurahia na kufaidika na
huduma zao ikiwemo kutoa elimu juu ya umuhimu wa matumizi ya mifumo ya
digitali katika kupata huduma kwa usalama wa fedha zao.
Akifafanua
zaidi, Mkuu wa Biashara ya Kadi wa Benki ya NMB- Philbert Casmir
amesema kuwa, Benki hiyo imekuja kivingine Msimu huu wa Sikukuu kwa
kuhakikisha wateja wao wanafaidika kupitia kampeni zao za ‘NMB Fri-Yay’
na MastaBata Sio Kikawaida.
“NMB inatambua kila siku lazima
wateja wetu wafanye huduma mbalimbali ikiwemo kupata chakula, kujaza
mafuta katika magari yao na kufurahia, na kupitia ‘NMB Fri-yay’ kila
ijumaa ya mwisho wa mwezi kila anaelipa kupitia kadi zao za NMB
Mastercard na Mastercard QR atapata punguzo hadi la asilimia 15,
wakinunua bidhaa katika vituo vya mafuta vilivyoainishwa na hiyo ni
pamoja na sehemu za vyakula na maeneo ya starehe ambayo tumeingia ubia
na wafanyabiashara katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Dodoma,
Mwanza na Zanzibar. Tunaimani kampeni hizi zitawapeleka wateja katika
njia ya kidigitali na kutunza miamala yao ya kibenki.”
Amesema hiyo yote ni katika
kuwatoa wateja katika mfumo wa matumizi ya fedha taslimu katika kufanya
manunuzi na kutumia mfumo wa kadi katika kufanya malipo ya huduma njia
ambayo ni rahisi na salama zaidi.
Ameeleza kuwa, katika msimu huu
wa sikukuu, wanahakikisha wateja wao wanafurahia sikukuu za mwisho wa
mwaka kwa kununua bidhaa na kutembelea sehemu mbalimbali kupitia kampeni
ya ‘MastaBata sio kikawaida’ kampeni iliyoifanya benki hiyo kuendelea
kuwa kinara kwa kuwazawadia wateja wao.
“Kupitia kampeni hii tunatoa
zawadi kwa wateja wetu pamoja na kutoa elimu ya kuacha matumizi za fedha
taslimu njia ambayo ni gharama na si salama na kugeukia matumizi ya
kadi katika kufanya huduma.” Amesema Philbert.
Ameeleza kuwa kampeni ya
‘MastaBata Sio Kikawaida’ ni ya muda wa miezi mitatu ikiwa na zawadi za
wiki, mwezi na zawadi za mshindi wa jumla. Nayo pia ikiwalenga
wanaotumia kadi za NMB Mastacard na Mastacard QR kufanya manunuzi.
“Katika zawadi za wiki, kila
wiki kuna washindi 40 wanajishindia laki moja kila mmoja, zawadi za
mwezi ni simu ya kisasa aina ya Samsung Galaxy note 20 na zawadi kubwa
ya mwisho ya kumalizia kampeni ni kuwapeleka wateja wetu kutembelea
vivutio mbalimbali zikiwemo mbuga za wanyama za Serengeti, Ngorongoro
na Visiwa vya karafuu visiwani Zanzibar.” Amesema.
Aidha amesema kuwa hiyo ni katika kudumisha utalii wa ndani wateja watapata huduma za hadhi ya nyota tano.
“Na tumeiita ‘MastaBata Sio
Kikawaida’ kwa sababu mteja mwingine anaweza asisafiri au tayari
ameshatembelea maeneo ya vivutio basi atakuwa na machaguo, gharama
ileile ya kusafiri atachagua zawadi nyingine nyingi zikiwemo Televisheni
ya kisasa, jokofu, Microwave, Kompyuta mpakato na simu za mkononi na
hii yote ni katika kuwazawadia wateja wetu na kujenga uelewa wa umuhimu
wa kutumia kadi za NMB Mastercard na Mastercard QR inayopatikana kupitia
NMB Mkononi.” Amesema.
NMB
ina wateja zaidi ya milioni tatu wenye kadi na inawasihi waendelee
kuzitumia ili waweze kunufaika na hizi ofa hasa msimu huu wa Sikukuu
lakini wajijengee mazoea ya kutotumia pesa taslimu(keshi).
No comments :
Post a Comment